NAMNA ya kujipanga katika kukaa ukumbini wakati wa tuzo ilizingatia herufi zao hivyo Iniesta akajikuta akikaa katikati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Lakini hakuna kati yao wapinzani hao wakubwa aliyempigia kura mwenzake. "Kwanini?" unaweza kujiuliza... majibu ni haya hapa...
Messi alidai kwamba wazo lake lilikuwa ni kuwapigia kura mchezaji mwenzake wa Barcelona na ndiyo maana akawachagua Xavi na Iniesta. Chaguo lake la tatu, lilikuwa mchezaji mwenzake wa timu ya taifa, Aguero. Hata hivyo... "Ingekuwa ni ujinga kutomfikiria Cristiano kama mmoaja wachezaji bora. Nilifikiria tu kwamba hawa ndiyo wachezaji ninaopaswa kuwapigia kura," alisema Messi.
Cristiano Ronaldo alikuwa na sababu nzuri zaidi. Licha ya kuwa ni nahodha wa timu ya taifa ya Ureno hakuweza kupiga kura. Alikuwa majeruhi. "Niliumia wakati nikiwa na timu ya taifa hivyo nikarudishwa nyumbani. Sikupiga kura," alifafanua.

إرسال تعليق