Maelfu wajazana madukani kununua Silaha Kabla ya Kupitishwa kwa Sheria Mpya!!

Siku ya Jana kumeshuhudiwa misururu ya Foleni huko Nchini Marekani katika maduka ya Silaha Hususani Bastola na Bunduki ambapo wengi miongoni mwa wateja hao wamesema kwamba wameamua kufanya manunuzi hayo haraka kabla ya kupitishwa kwa sheria mpya ambayo inatarajiwa kuwabana wanunuzi na watumiaji wa silaha nchini humo.
      Kuundwa kwa sheria hiyo kunatokana na shinikizo kutoka serikalini, wazazi na jumuiya za haki za kibinadamu kufatia mauaji yalifanyika mwezi Desemba mwaka 2012 ambapo kijana Adam Lanza aliua wanafunzi 26 wa shule ya Msingi ya Connectcuit  pamoja na mwalimu wao ambaye alikuwa mama yake mzazi na kisha yeye mwenyewe kujiua.

Post a Comment

Previous Post Next Post