Maisha ya Mali: Mchanganyiko wa faraja na mashaka.

Waislamu wenye itikadi kali wanaojiita walinzi wa dini, Ansar Dine, waliudhibiti mji wa Gao kaskazini mwa Mali kwa muda wa nusu mwaka. Baada ya kuwatimua washirika wao wa hapo awali, waasi wa Tuareg, wapiganaji wa Ansar Dine walianza kuzitumia sheria za Kiislamu.
 Lakini sasa watu katika mji wa Gao na mingine ya kaskazini mwa nchi hiyo wameanza kupata utulivu baada ya wapiganaji hao wa Kiislamu kutimua mbio kufuatia mashambulizi ya ndege za Ufaransa.
 Licha ya hisia za faraja kuonekana miongoni mwa wakaazi hao wa kaskazini, hata hivyo watu hao pia wana wasiwasi, kwa sababu mgogoro wa nchi yao bado haujamalizika licha ya hatua za kijeshi zinazochukuliwa na Ufaransa.
 “Sasa hali ni shwari. Watu wanatoka majumbani mwao kuvuta sigara nje bila ya usumbufu. Hata hivyo, muda mfupi uliopita ndege zilishambulia karibu na hapa. Lakini hakuna raia yeyote aliyedhurika. Baadhi ya wapiganaji wa Kiislamu bado wapo, lakini hawatoki nje ya magari yao,” anasema mmoja wa wakaazi hao.

Post a Comment

Previous Post Next Post