
Wanajeshi wa Ufaransa wanasema wameukomboa mji wa mwisho uliokuwa ngome ya wapiganaji wa kiisilamu
Wanajeshi wa Ufaransa, wanasema 
kuwa wamefanikiwa kuingia katika mji wa waasi wa Kidal, ambao ndio ngome
 ya mwisho ya wapiganaji hao.
Huu ndio mji wa mwisho mkubwa ambao walilenga kuukomboa kutoka mikononi mwa wapiganaji.Wapiganaji wa kiisilamu waliriarifiwa tayari kuondoka mji humo na sasa ni wazi kuwa wanajeshi nduio wanaudhibiti.
Majeshi ya Mali na Ufaransa yamekuwa yakiwasaka waasi hao katima maeneo ya Kaskazini na hata kukomboa miji ya Gao na Timbuktu bila ya upinzani wowote. .
Ufaransa ambayo ni koloni ya zamani ya Mali, ilianza harakati za kijeshi mwezi huu baada ya wapiganaji wa kiisilamu kuonekana kuwa tisho kubwa katika maeneo ya Kusini.
'Kuangamiza Ugaidi'
Msemaji wa jeshi la Ufaransa kanali, Thierry Burkhard alithibitisha kuwa wanjeshi wa Ufaransa walishika doria katika eneo la Kidal usiku kucha Kidal".
Wapiganaji wa kiisilamu waliokuwa wandhibiti Kidal
"wanajeshi hao wanashika doria kwa usaidizi wa helikopta''
Mji wa Kidal,ambao uko umbali wa kilomita 1,500 kaskazini mashariki mwa Bamako, hadi ulipokombol;ewa ulikuwa chini ya udhibiti wa kundi la wapiganaji wa Ansar Dine.
Wapiganaji hao walitoroka Timbuktu ingawa walifaya kitendo cha kulipiza kisasi kabla ya kuondoka.
Hata hivyo, vuguvugu la Islamic Movement of Azawad (IMA), ambalo hivi karibuni,lilijitenga na makundi mengine ya wapiganaji, sasa linadhibiti Kidal, ingawa wapiganaji wa Tuareg pia wanadai kuudhibiti mji huo.
إرسال تعليق