Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akinunua mishikaki kwa mmoja wa wauzaji
wa vyakula mbalimbali husuasan nyama, baada ya kuwasili na msafara wake
stesheni ya Saranda, mkoani Singida, leo mchana. Kinana na msafara wake
wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, wanasafiri kwa treni kutoka Dar es
Salaam, kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM. (Wapili kulia
ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai.
Makatibu
wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro
(kulia) na wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wapili kulia) wakinunua
chakula kwa mamalishe, kwenye stendi ya Saranda mkoani Singida, daaba ya
kuwasili kwenye stesheni hiyo, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM
ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari
yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za
miaka 36 ya CCM.
Katibu
wa NEC, Siasa na Uhusiano wa KImataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Naibu
Katibu Mkuu wa CCM, Mstaafu John Chiligati wakishiriki kucheza ngoma ya
wakazi wa mkoa wa Singida, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM
ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari
yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za
miaka 36 ya CCM. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Martine Shigela.Picha na
Bashir Nkoromo
إرسال تعليق