Aliyekuwa Raisi Wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha Idd
Mohammed (Wa Sita kutoka Kulia Waliokaa Kwenye Viti) Alipokuwa Kwenye
moja ya Kampeni zake za Kuwania Kiti Cha Uraisi Mwaka Jana Chuoni Hapo
Aliyekuwa Raisi Wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii,Sanaa na Lugha Cha Chuo
Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ambaye pia ni Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 wa Kozi
ya Biashara na Akaunti (BCOM Accounting) Idd Mohammed mnamo alhamisi
alishikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma katika Kituo Cha Polisi
Cha UDOM kwa tuhuma za Wizi wa Pesa Za Kitanzania Shilingi Milioni 15.6
mali ya serikali ya wanafunzi wa kitivo hiko ambazo aliweza kuhamisha
kutoka Kwenye Akaunti ya Serikali ya Wanafunzi wa Kitivo Hiko Kwenda
kwenye Akaunti Binafsi ya Waziri Wa Fedha Wa Kitivo Hiko Ibrahim Matata.
Raisi huyo pamoja na Waziri wake wa fedha walikamatwa jana alhamisi na
Polisi huku wakikutwa na Pesa taslimu shilingi Milioni 7,224,000 ambazo
walikutwa nazo mikononi. Chanzo chetu kilienda kusema kuwa Awali Raisi
huyo inasemekana aliwaweka watia saini anaowataka yeye kinyume na
taratibu na kuwatoa waliowekwa kwa taratibu na Sheria za Bunge la
Serikali ya Wanafunzi wa Kitivo hiko kuwa ndio watu wenye dhamana ya
kuruhusu pesa za Serikali ya Wanafunzi kutoka Katika Akaunti hiyo ya
Serikali ya Wanafunzi.
Chanzo Chetu kiliendelea Kutupasha kuwa Raisi huyo pamoja na Waziri wake
wa Fedha walikamatwa Jana na kulala katika Kituo Cha Polisi Cha UDOM
tayari kwa Uchunguzi na hatua za kisheria Kuchukuliwa dhidi yao kabla
hawajaweza kutoka jana Kwa dhamana.
Habari zaidi ambazo Lukaza Blog imezipata kutoka katika Vyanzo tofauti
tofauti Zinadai kuwa Raisi huyo pamoja na Waziri wake Wa fedha wanaweza
kufikishwa Mahakamani Jumatatu kwaajili ya kusomewa mashtaka yao ikiwemo
tuhuma za wizi wa Shilingi Milioni 15.6 ambazo walikutwa nazo mkononi
na kiasi kingine kubaki kwenye akaunti Binafsi ya Waziri Huyo wa Fedha
Ibrahim Matata
Baada ya Bunge la Serikali ya Wanafunzi wa Kitivo Hiko Cha Sayansi ya
Jamii, Sanaa na Lugha kukaa jana Majira ya Saa Kumi Jioni nakuweza Kutoa
uamuzi wa Kumvua Madaraka Raisi huyo ambapo imepelekea Baraza zima la
Mawaziri kuvunjwa na kupelekea Spika Wa Bunge Kushikilia Serikali Hiyo
Kwa Muda.
"Kwenye Majira ya Saa 10 jioni ya leo (Jana) bunge lilikaa na ndipo
Spika alipoamua kuchukua uamuzi uliotolewa na wabunge wa kumvua madaraka
raisi huyo na kupelekea Baraza la mawaziri kuvunjwa na Serikali
kushikiliwa na Spika Wa Bunge hilo" Kilisema Chanzo Chetu.
Kwenye Majira ya Saa Moja Jioni ya jana aliyekuwa raisi wa Kitivo Hiko
Idd Mohammed na aliyekuwa waziri wa fedha Ibrahim Matata Waliweza
kuachiwa kwa Dhamana na Sasa Wapo Nje Kwa Dhamana
Chanzo Chetu kiliendelea kudai kuwa Kuna fununu zilizozagaa kwa baadhi
ya wanafunzi wachache wa kitivo hiko Kuwa Inasemekana Aliyekuwa Raisi Wa
Kitivo Hiko ana kashfa ya Kuomba Rushwa ya Shilingi Milioni Moja laki
moja na hamsini elfu ( 1,150,000 ) katika Duka lililopo bweni namba 13
(block 13) ambapo chanzo hiko kimedai kuwa kulikuwa na ushahidi wa Sauti
ambao ulirekodiwa wakati Mtuhumiwa huyo akiomba rushwa kabla ya
kukamatwa hapo juzi kwa tuhuma za Wizi wa Shilingi Milioni 15.6 akiwa na
aliyekuwa waziri wake wa fedha Ibrahim Matata
إرسال تعليق