Rais Shirikisho la Filamu Tanzania (TFF), Simon Mwakifamba akiongea mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).
Msanii Vitalis Maembe akionyesha mfano atakavyokamua siku hiyo.
Dude akitoa kionjo cha nyimbo yake atakayoitambulisha kwa mara ya kwanza siku hiyo.
Baadhi ya wasanii hao wakisikiliza mawaidha kutoka kwa rais wao.
Waandishi wa habari wakichukua matukio ya ishu hiyo.
RAIS
wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TFF), Simon Mwakifamba, amezungumzia
juu ya maandalizi ya tamasha la wasanii wa filamu Bongo, walivyojiandaa
kwa makamuzi ya nguvu Jumamosi hii ndani ya Ukumbi wa Dar Live uliopo
Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
mbele ya wanahabari, katika viwanja vya Leaders Club leo, Mwakifwamba
alisema maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na kila kilichopangwa
kitafanyika. Katika upande wa burudani, kutakuwa na wasanii mbalimbali
waliojitolea kusapoti tamasha hilo ambao ni Vitalis Maembe, Mrisho
Mpoto, Scorpion Girls, Dude, Mtunisi, Radon, Ray, JB, Wema, Jack Wolper,
Uwoya, Dk Cheni, na wengine kibao.
(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)
إرسال تعليق