Jamaa
mmoja mkazi wa Portland katika jimbo la Oregon nchini Marekani
amekamatwa akituhumiwa kwa makosa kadhaa iliwemo kufanya vurugu nyumbani
baada ya kudaiwa kumnyonga mpenzi wake kwa kutumia rasta zake
‘dreadlocks’.
Kwa
mujibu wa taarifa za polisi wa Portland, maafisa usalama walipokea
ripoti kuhusu kuwepo vurugu katika nyumba, hata hivyo walipofika jamaa
huyo alishatoweka na kumuacha mpenzi wake akiugulia maumivu.
Mwanamke
huyo amewaambia polisi hao kuwa mpenzi wake Caleb Grotberg alikuwa
amemshambulia kwa kipigo na kumyonga akitumia rasta za kichwani kwake.
Hata hivyo jamaa huyo alikamatwa muda mfupi katika maeneo jirani ya mji huo.
Caleb
Grotberg mwenye umri wa miaka 32, amefunguliwa mashitaka mbalimbali ya
kihalifu, ikiwemo kunyonga, kushambulia mwili na utekaji.
Mo Blog: Jamani hii ni kivingine zaidi, wenye ‘dredlocks’ tafadhalini bwana.
إرسال تعليق