 |
Mgeni
rasmi,
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho
akisalimiana na kiungo wa Simba SC, Jonas katika mchezo wa leo wa Nusu
Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Amaan,
Zanzibar. Azam ilishinda kwa penalti 5-4 kufuatia sare
ya 2-2 ndani ya dakika 120.
|
 |
Mgeni
rasmi,
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho
akisalimiana na kipa
wa Azam FC, Mwadini Ally katika mchezo wa leo wa Nusu Fainali ya Kombe
la Mapinduzi dhidi ya Simba SC kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam
ilishinda kwa penalti 5-4 kufuatia sare
ya 2-2 ndani ya dakika 120.
|
 |
| Kikosi cha Simba leo |
 |
| Kikosi cha Azam leo |
 |
| Kipre Balou wa Azam kulia akiwania mpira wa juu na Abdallah Seseme wa Simba |
 |
| Samir Hajji Nuhu wa Azam akiwatoka wachezaji wa Simba |
 |
| Miraj Adam wa Simba akiuwahi mpira dhidi ya Hajji Nuhu wa Azam |
 |
| Humphrey Mieno wa Azam aliyeenda hewani kuifungia bao la kwanza timu yake |
 |
| Wachezaji
wa Azam, Ibrahim Mwaipopo kushoto na Uhuru Suleiman kulia wakimdhibiti
kiungo wa Simba SC, Ramadhani Singano 'Messi' katikati huku kocha wake
Jamhuri Kihwelo 'Julio' kulia kabisa akishuhudia |
 |
| Wachezaji wa Azam wakimpongeza Humphrey Mieno kufunga bao la kwanza |
 |
| Paul Ngalema wa Simba akimdhibiti Uhuru Suleiman wa Azam FC |
 |
| Ibrahim Mwaipopo anatoa pasi huku akiwa amebanwa na wachezaji wa Simba SC |
 |
| Kipa
wa Simba SC, William Mweta akiwa amedaka mbele ya mshambuliaji wa Azam,
Brian Umony huku beki wake Paul Ngalema akiwa tayari kutoa msaada kulia |
 |
| Seif Abdallah wa Azam akiwatoka mabeki wa Simba |
 |
| Ramadhani Mkipalamoto akiwatoka mabeki wa Azam |
 |
| Kipre Balou akimiliki mpira mbele ya Jonas Mkude wa Simba |
 |
| Haruna Chanongo akitoa pasi kwa kichwa mbele ya Ibrahim Mwaipopo |
 |
| Miraj Madenge wa Simba, akimiliki mpira mbele ya Himid Mao wa Azam |
 |
| Himid ameosha mbele ya Madenge |
 |
| Madenge akimpongeza Rashid Ismail kufunga bao la kwanza la Simba SC |
 |
| Mwadini Ally amedaka mbele ya beki wake Himi Mao, huku Ramadhani Mkipalamoto akifukuzia |
 |
| David Mwantika wa Azam akimdhibiti Mkipalamoto wa Simba SC |
 |
| Samih Hajji Nuhu amempitia Mkipalamoto na mpira wake |
 |
| Daktari wa Simba SC akimtoa nje beki Hassan Hatibu baada ya kuumia kiasi cha kushindwa kuendelea na mchezo |
 |
| Mkipalamoto amemlamba chenga Himid Mao, anaondoka... |
 |
| Lakini shuti lake lilidakwa na Mwadini...lilikuwa bao la wazi sana alikosa |
 |
| Gaudence Mwaikimba akipiga mpira kichwa ambao ulitoka nje sentimita chache |
 |
| Hatari langoni mwa Simba SC |
 |
| Lakini salama... |
 |
| Himid Mao akiwa ametoa mpira nje kupunguza kasi ya Haruna Chanongo wa Simba SC |
 |
| Mwantika amezuia, anaanza kugeuka taratibu |
 |
| Miraj Madenge akishangilia baada ya kuifungia Simba bao la pili |
 |
| Kutoka kulia ni Hassan Khatibu na Rashid Ismail wakicheza na Miraj Madenge kumpongeza kwa kufunga bao la pili |
 |
| Mkipalamoto akitafuta mbinu za kumtoka Mwantika |
 |
| Hapa ni wakati Azam ikiwa nyuma kwa 2-1, tazama sura ya kocha wa Azam, Muingereza Stewart Hall ilivyokuwa |
 |
| Brian Umony akiwa benchi baada ya kutolewa |
 |
| Kipa
wa Simba SC, William Mweta akigagaa mpira ukiwa nyavuni...ni baada ya
mkwaju wa penalti wa Joackins Atudo kuipatia Azam bao la kusawazisha |
 |
| Wachezaji wa Azam Seif Abdallah kulia na Humphrey Mieno kushoto wakiwa kwenye benchi baada ya kutolewa |
 |
| Makocha wanne wa kigeni wa Azam wakiwapa mawaidha wachezaji wao kabla ya kuingia kumalizia dakika 30 za nyongeza |
 |
| Kuna
wakati ilibidi Stewart Hall aombe ushauri kwa mchezaji wake wa akiba,
Luckson Kakolaki kushoto ambaye anamuambia cha kufanya, bila shaka
ilikuwa ushauri mzuri na ndiyo maana timu ilishinda |
Picha zote Na:- Bin Zubeiry
 |
| Shujaa wa Azam, Malikqa Ndeule akiwa amebebwa juu juu |
إرسال تعليق