Ujumbe wa Tucta wafika Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwasilisha Maoni ya Katiba Mpya.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Edmund Mvungi (katikati) akizungumza na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) waliofika katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume Jijini Dar es Salaam jana  (Jumatano, Januari 9, 2013) kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Mjumbe wa Tume, Bi. Maria Kashonda na katikati ni Katibu Mkuu wa TUCTA, Bw. Nicholus Mgaya.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) Bw. Nicholus Mgaya (kushoto) akizunguma wakati wa mkutano baina yao na Uongozi wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika Makao Makuu ya Tume Jijini Dar es Salaam, ambapo TUCTA iliwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Wajumbe wa Tume, Dk. Edmund Mvungi na Bi. Maria Kashonda.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Maria Kashonda (kulia) akizungumza na Viongozi   wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) waliofika katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume Jijini Dar es Salaam  jana kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TUCTA Bw. Nicholus Mgaya. Katikati ni Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Edmund Mvungi.

Post a Comment

أحدث أقدم