VAN PERSIE AELEZEA SIRI YAKE YA KUPIGA MABAO MAN UTD

 
LONDON, ENGLAND
ROBIN VAN PERSIE amesema kuwa imekuwa kazi rahisi kwake kupiga mabao kwa sababu amezungukwa na mabingwa katika klabu ya Manchester United.
Mshambuliaji huyo aliongeza mabao mawili katika kapu yake siku ya Mwaka Mpya na kufanya jumla ya mabao 19 kwa msimu huu.
Van Persie alisema: “Namshukuru kocha, wachezaji wenzangu na wafanyakazi wote United — kila mmoja amekuwa msaada na kufanya mambo kuwa rahisi sana kwangu.

“Nahisi nimezungukwa na mabingwa. Wanajua jinsi ya kushinda na hilo hakika linafanya mambo yawe rahisi kwangu.
“Ilikuwa hivyo leo (Jumanne usiku). Kwa bao langu la pili, Danny Welbeck angaliweza kufunga, lakini alipita.”
Van Persie pia amempongeza Javier Hernandez, ambaye alipiga mabao mengine mawili katika ushindi wa 4-0 nyumbani kwa Wigan.
Mdachi huyo alisema: “Alitoa pasi nzuri kwa kweli kwa bao langu la kwanza.

Post a Comment

أحدث أقدم