John
Bukuku Mkurugenzi wa Fullshangweblog akiwa katika picha ya pamoja na
David Milliband aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Mbunge wa
jimbo la South Shield na mmoja wa wamiliki wa klabu ya Sunderland ya
Uingereza wakati alipotembe klabuni hapo kikazi mwezi Oktoba mwaka jana.
……………………………………………………………………….
Napenda
kutoa shukurani zangu za mwaka 2013 kwa makampuni na wadau mbalimbali
waliotusapoti katika kuendeleza umuvuzishaji au kurusha matukio
mbalimbali yanayotokea ndani na nje ya nchi katika mtandao wetu wa
kijamii www.fullshangweblog.com kwa ushirikiano wao waliotupa wakati
wote katika kipindi cha miaka minne toka tuzaliwe rasmi 2008.
Sapoti hii imetupa moyo wakujituma
zaidi katika kazi lakini pia imetuwezesha kugharamia baadhi ya gharama
za muhimu katika utendaji wetu wa kazi za kila siku, na kutupa jeuri
angalau ya kuthubutu kupata glasi ya juisi au kikombe cha kahawa wakati
tukiwa katika kompyuta zetu tukimuvuzisha matukio.
Hili
si jambo dogo ni jambo la kutia moyo kwani mmethamini kile
tunachokifanya kwa ajili ya kuelimisha jamii, kupasha habari na kukosoa
mambo yanapokwenda ndivyo sivyo, Pia tumeweza kusafiri ndani na nje ya
Tanzania kwa ajili ya kukusanya matukio mbalimbali yote ni kuokana na
msaada mkubwa kutoka kwenu wadau.
Naomba
nitaje baadhi ya Kampuni na wadau waliotusaidia kwa namna moja au
nyingine katika ushauri wa hali na mali nikianza na Kampuni ya bia ya
Serengeti (SBL) kupitia aliyekuwa mkurugenzi wa Kampuni hiyo Richard
Wells, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw. Steve Ganon, Mkurugenzi wa Masoko
wa Kampuni hiyo Ephraim Mafuru, Mkurugenzi wa Mawasiliano Nandi
Mwiyombela, Meneja wa Mawasiliano Imani Lwinga, Meneja wa Bia ya
Serengeti Allan Chonjo na wafanyakazi wote wa kampuni ya bia ya
Serengeti
Napenda
kutoa shukurani kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya NBC Lawrence
Mafuru, Mwinda Kiula Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Aden Kitomari Meneja
wa Matangazo na Eddie Muhina Meneja Mahusiano, kwa ushirikiano waliotupa
tunasema asante sana na tuko pamoja katika ushirikiano huu mzuri kwa
maendeleo ya ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.
Shukurani pia ziende kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano Benki ya NMB, Imani Kajula , Meneja Mawasiliano Josephine Kulwa
na Elizabeth Ikengo kwa ushirikiano ambao tumekuwa tukipata kutoka kwa
benki hiyo na wafanyakazi wote kwa ujumla tunasema asanteni sana wadau.
Natoa pia shukurani kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Bayport Finacial Services Ngula Cheyo na
viongozi pamoja na wafanyakazi wote wa taasisi hiyo , Viongozi na
wafanyakazi wote wa Mfuko wa Afya ya Jamii (NHIF) pamoja na wafanyakazi
wote na Mkurugenzi wa Kampuni ya Wilna International ya Japani Willy Ngoya
kwani hawa wote tunawashukuru kwa sapoti waliyotupa kwa muda wakati
ambao tumekuwa tukishirikiana nao, tunasema “Asanteni sana wadau”
Shukurani za pekee zimwendee Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Montage Limited ya jijini Dar es salaam Teddy Mapunda
kwa ushirikiano alionipa kwakweli ninajisikia furaha kufanya kazi na
Mapunda, kwani amekuwa mshauri na msaada mkubwa kwa hali na mali katika
kuhakikisha Mablogger tunasonga mbele katika kazi zetu za kila siku”
niwape siri wakati nikihudhuria mikutano yake ya habari aliwahi
kuniuliza mbona sina (Laptop) kompyuta ya mkononi na kazi zangu
nazifanyia wapi” Aliniuliza Teddy.
Nilimjibu
nafanyia kwenye ‘Inernet Cafe’ kutokana na majibu hayo aliguswa sana
hivyo alinipa shilingi milioni moja kwa ajili ya kununulia kompyuta.
“mkutano ujao nitakaofanya uje na kompyuta hiyo” Alisistiza Mapunda.
Kwa
kweli Sina cha kuilipa Familia ya Nesto Mapunda ,mkeweTeddy Mapunda
kutokana na kuwa sehemu kubwa ya mafanikio ya Shughuli zangu za
kuendesha Mtandao wa www.fullshangweblog.com mungu awabariki.

إرسال تعليق