ASKARI WA FFU ANAYETUHUMIWA KUFANYA MAUWAJI YA MWANGOSI MAHAKAMANI LEO


mwili  wa marehemu Mwangosi  ukikanywagwa na askari waliokuwa  wakimsaidia mwenzao aliyejeruhiwa kwa bomu  lililomuua Mwangosi
ASKARI  kikosi cha kituliza ghasia (FFU )mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) anayetuhumiwa  kumuua  aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi kupandishwa tena kizimbani leo katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa.
Mtuhumiwa  huyo  leo anatarajia  kufikishwa tena mahakamani huku tayari mahakama hiyo chini ya hakimu Dyness Lyimo ikiwa imetoa onyo kwa askari  waliomfikisha mahakamani hapo mara ya mwisho  kutokana na kitendo cha kuidharau mahakamani  hiyo kwa kumtoa mtuhumiwa huyo ndani ya chumba cha mahakama kabla ya shughuli za mahakama kuhitimishwa .
Askari hao na mtuhumiwa  walionyesha kuidharau mahakamani  hiyo kwa kumtoa mtuhumiwa huku  mahakama ikiwa inaendelea na kupelekea hakimu kumwagiza wakili wa serikali kuwafuata askari hao na mtuhumiwa ili kurudi ndani ya chumba hicho na kuwahoji askari hao kwa kitendo walichokifanya kabla ya kuomba msamaha .

Kesi hiyo namba   namba 1 ya mwaka 2012 ya mauwaji hadi  sasa mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo zaidi ya mara nne na kesi hiyo ikiendelea  kutajwa .
Mtuhumiwa  huyo anatuhumiwa  kumuua kwa  kwa   bomu aliyekuwa  mwandishi  wa habari wa Chanel Tena  mkoa  wa Iringa  marehemu Mwangosi  septemba 2 Septemba mwaka jana  katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa  wakati  wa vurugu kati ya  polisi na wafuasi wa  Chadema .kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai. Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002,

Post a Comment

أحدث أقدم