Dr. Nchimbi: Kuuwawa kwa Padri huko Zanzibar si Ujambazi bali ni Ugaidi!


PADRI wa kanisa katoliki jimbo la Zanzibar,amepigwa risasi za kichwa na kifuani na kuuwawa na watu wasiojulikana.

Padri huyo aliyetambuliwa kwa jina la Evaritus Gabriel Mushi wa kanisa katoliki parokia ya mtakatifu Joseph Shangani mjini , Zanzibar

Watu hao ,ambao hawajafahamika wala kukamatwa ,walifanya unyama huo jana saa 12 Alfajiri asubuhi nje ya kigango cha mtakatifu theresia kanisa la mtoni,wakati akijiandaa kushuka kwenye gari kuingia kanisani kufanya maandalizi ya ibada ya jumapili.

Akizungumza na waandishi wa habari kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa Alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Alisema kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa jeshi hilo Padri Mushi ,alipigwa risasi akiwa kwenye ndani ya gari na kujeruhiwa vibaya sehemu za kichwa na kifua.
Alisema baada ya kutokea kwa tukio hilo punde baadhi ya waumini wa kanisa hilo waliofika katika kanisa hilo kwa ajili ya ibada walimpeleka Padri Mushi katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya matibabu baada ya muda mchache Akafariki

Post a Comment

أحدث أقدم