
Kiongozi wa zamani wa Libya Moammer Gaddafi,ambaye aliondolewa madarakani kwa mapinduzi yaliyofanywa na raia nchini humo.
Na Martha Saranga Amini
Majeshi ya Ulinzi nchini Libya yameimarisha ulinzi zaidi katika siku
ambazo taifa hilo la Afrika kaskazini linaadhimisha miaka miwili tangu
kuanza kwa harakati zilizomwondoa madarakani kiongozi wa zamani kanali
Moammer Gaddafi.
Raia hao walipeperusha bendera huku kauli mbiu mbalimbali zikisikika
kuyasifu mapinduzi ya libya wakati magari yalizunguka mijini humo kama
sehemu ya shangwe hizo sambamba na ving'ora kusikika.
Huko Benghazi raia walimiminika barabarani wakifanya matembezi ya pamoja
wakikumbukia siku na eneo ambalo harakati hizo zilianzia mnamo miaka
miwili iliyopita wakiwasifu walioaga dunia na kujeruhiwa katika harakati
za kuumaliza utawala wa kanali Gaddafi.
Maadhimisho ya mapigano ambayo yalimalizika kwa mauaji ya Kadhafi mnamo
Oktoba 2011 yanakuja wakati utawala mpya wa Libya ukikabiliwa na vita
mpya dhidi ya wakosoaji ambao wametoa wito wa kufanyika mapinduzi mapya
na kuushutumu utawala kushindwa kutekeleza suala la mageuzi
walilolihitaji.
Via kiswahili.rfi.fr
إرسال تعليق