|
Mwenyekiti
wa CCM Rais
Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete
akipigira
kura kuchagua
wajumbe
wa Kamati kuu ya
Halmashauri
Kuu ya Taifa katika
ukumbi wa White House uliopo
makao
makuu ya CCM mjini
Dodoma
.
|
Halmashauri Kuu ya
Taifa ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao chake cha siku mbili Februari 10 na
11, 2013 kilichofanyika mjini Dodoma, pamoja na mambo mengine kimeridhia uteuzi
na kufanya uchaguzi wa Wajumbe 14 wa Kamati Kuu yake.
Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM imeridhia uteuzi wa Dokta Salim Ahmed Salim kuwa Mjumbe wa
Halmashauri Kuu kupitia nafasi 10 za uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM.
Wajumbe 14
waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni:-
Wajumbe
wa Kamati Kuu - Bara.
1. Ndugu Pindi Chana - Mbunge wa Viti Maalum.
2. Ndugu Adam Kimbisa - Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma.
3. Ndugu William Lukuvi - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge).
4. Dokta Emmanuel Nchimbi- Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
5. Ndugu Jerry Slaa - Meya wa Manispaa ya Ilala.
6. Profesa Anna Tibaijuka- Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
7. Ndugu Stephen Wassira - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu).
Wajumbe wa Kamati Kuu - Zanzibar.
|
Baadhi
ya wajumbe wa
Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa
wakipiga kura zao kuwachagua
wajumbe
wa Kamati kuu
mjini
Dodoma katika
ukumbi
wa White House
|
1. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha- Waziri wa Ulinzi.
2. Ndugu Hussein Mwinyi - Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
3. Profesa Makame Mbarawa Mnyaa - Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
4. Dokta Salim Ahmed Salim
5. Ndugu Maua Daftari - Naibu Waziri wa zamani wa Mawasiliano na Uchukuzi.
6. Ndugu Samia Suluhu Hassan-
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano)
7. Ndugu Hadija H. Aboud.
Wajumbe
hao wapya wanaunda Kamati Kuu pamoja na wengine wanaoingia kwa nyadhifa zao.
Imetolewa
na:-
Nape Moses Nnauye,
KATIBU
WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI
NA UENEZI
12/02/2013
Post a Comment