Wilvina Mkandala (24) akitolewa mahakamani mara tu baada ya kusomewa hukumu ya kifungo cha maisaha
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
WILIVINA
MKANDALA mwenye umri wa miaka 24 ameukumiwa kutumikia kifungo cha
maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumlisha mtoto ANETH GASTO
mwenye umri wa 5 mitano kinyesi na na kumuunguza kwa maji ya moto
Akisoma
hati ya mashtaka mwendesha mashtaka wa serikali ACHIREY MULISA ameiomba
mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa watu
wegine wenye tabia kama hiyo
Akisoma
hukumu hiyo kwa muda wa dakika hamsini hakimu mfawidhi wa mahakama ya
wilaya mbeya GILBERT NDEURUO ameridhishwa na na ushahidi uliotolewa na
upande wa Jamuhuri kwamba mshtakiwa amtenda kosa kinyume cha sheria
cha makosa ya jinai namba 222(a)sura ya kumi na sita ya marekebisho ya
mwaka 2002
Hata
hivyo ameiomba serikali kutunga sheria ya kumlinda mtoto kutokana na
vitendo vilivyokithiri kwa watoto ambapo amesema tanzania haina sheria
ya kulinda mtoto. Akijitetea
mahakamani mtuhumiwa huyo ameiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani
anategemewa na familia sababu ambazo zilipingwa na mahakama hiyo

Mtoto Aneth akionesha alivyoumizwa vibaya na kuunguzwa mkono huu ambo ilibidi ukwate
Baadhi ya wakazi wa majengo mashuhuda na majirani alipokuwa anaishi mtuhumiwa wakimsifu hakimu kwa hukumu aliyotoa kwa mtuhumiwa huyo.
إرسال تعليق