
Mratibu
wa timu ya Kijitonyama Veterans, Majuto Omary akimtoka mchezaji wa timu
ya Kombaini ya Tabora, Ibrahim Masoud “Maestro” katika moja ya mchezo
wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Kijitonyama. Timu hizo zilitoka
sare ya bao 1-1 huku mabao yakifungwa na wachezaji hao wawili kwa
upande wa timu zao.
**********************************
Na Mwandishi Wetu
UONGOZI
wa timu ya Kijitonyama Veterans umepitisha azimio la kutocheza mechi
yoyote ya kirafiki dhidi ya timu ya Mbezi Veterans ya barabara ya
Morogoro kutokana na kile ilichokiita ‘tabia si ya kiwanamichezo’.
Kauli
hiyo ilitolewa na mratibu mkuu wa timu hiyo, Majuto Omary kufuatia
kitendo cha timu hiyo kushindwa kutokea uwanjani katika mchezo wao
maalum wa kirafiki uliopangwa kufanyika jana asubuhi kwenye uwanja wa
Kijitonyama.
Majuto
alisema kuwa mechi hiyo iliombwa na timu hiyo ya Mbezi na wao
(Kijitonyama) kuwakubalia kutokana na ukweli kuwa michezo ni afya mbali
ya kudumisha urafiki.
Alisema
kuwa mechi hiyo ilipangwa kuanza saa 2.00 asubuhi, na timu hiyo
ilithibitisha nusu saa kabla ya mechi hiyo kuwa wanakuja na wapo katika
maandalizi.
Alifafanua
kuwa baada ya hapo, viongozi wa timu hiyo hawakuonekana uwanjani na
mbaya zaidi hawakupokea simu zao walizokuwa wanapiga ili kujua
wamefikia wapi.
“Kinanchosikitisha
ni kwamba, walituweka hapo uwanjani na mbali ya kuwatumia ujumbe wa
simu ya mkononi kuwa wamefika wapi au wamekwama, hawakujibu chochote,
hii inaonekana kuwa ni makusudi,” alisema Majuto.
Majuto
ambaye pia ni kiongozi wa timu ya waandishi wa habari za michezo nchini
(Taswa FC), alisema kuwa hiyo si mara ya kwanza kwa timu hiyo kushindwa
kutokea uwanjani bila ya kutoa taarifa.
“Waliwahi
kuomba kucheza na Taswa FC pale Leaders Club, tukawakubalia, lakini
hawakutokea uwanjani na hata simu zetu wakawa hawapokei wala kujibu
ujumbe kusema kuwa wameshindwa kuja, walituacha uwanjani na kupoteza
muda, hii ni tabia yao,” alisema.
Alisema
kuwa haya maamuzi ni ya kudumu na watajaribu kuzitahadharisha na timu
nyingine kuhusiana na vitendo vya timu hiyo kwani ni vya kupotezea
muda wanamichezo.
إرسال تعليق