Alhamisi
hii feb7 2013 kuanzia saa moja usiku kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM
dakika 120 zitatumika kuirusha Exclusive interview ya BABU WA LOLIONDO,
hapa ni wakati nilipofika Loliondo… ni safari iliyochukua dakika 570
kutoka Arusha mjini, ni zaidi ya saa 9.

Safari
ya kwenda kwa Babu wa Loliondo Samunge ilianza kesho yake, hapa nilikua
kwenye defender ya polisi kwa sababu magari ya watu binafsi yalikua
yanagoma kwenda kutokana na vita kali ya Wasonjo na Wamasai, hivyo njia
pekee ya kufika kwa Babu ni kusindikizwa na Polisi ambao niliweka mafuta
kwenye gari yao, ni safari iliyochukua kama saa 5 kufika sababu njia
inayotumika ndio kwenye vita, tulipita eneo la vita, stori kamili ni
Alhamisi hii feb 7 2013 kwenye AMPLIFAYA Clouds Fm.

Nikiwa
kwenye interview ya zaidi ya dakika 60 na Babu wa Loliondo Ambilikile,
pichaz na stori nyingine zitapatikana hapa kwenye millardayo.com kuanzia
jumatano usiku na alhamisi, kwa sasa msikilize Babu wa Loliondo kwenye
hiyo promo yake hapo chini.

إرسال تعليق