
Kama ulikuwa mfatiliaji mzuri sana wa michezo ya olimpiki mwaka jana 2012 utamkumbuka Oscar Pistorius.

Alikuwa mwanariadha mlemavu kutoka Afika ya kusini aliyekuwa akionekana hivyo pichani pindi alipokuwa akikimbia.Alikimbia mbio za mita 400 na kushinda medali ya dhahabu.

Tukio hilo limetokea usiku Pretoria nyumbani kwake.Oscar mwenye miaka 26 na mpezi wake Reeva Steenkamp mwenye miaka 30 walianza kudate miezi miwili iliyopita.Inasemekana mwili wa mwanadada huyo ulikutwa na matundu ya risasi kichwani kifuani na mkononi na inasemekana amewaambia polisi amemuua kwa bahati mbaya baada ya kuhisi amevamiwa na majambazi nyumbani kwake kumbe ni mpenzi wake.Inahisiwa dada labda aliingia ndani kwa lengo la kumsuprise mpenzi kwa siku ya wapendanao na yeye kuhisi amevamiwa na kushoot.

Oscar alipokuwa akichukuliwa na polisi

Oscar Pistorius ni mwanamichezo mwenye ulemavu wa miguu.Hana miguu yote miwili lakini amekuwa
alama ya shujaa kwa walemavu wenzake.Amekuwa akipromote michezo kwa
walemavu na pia mlemavu maarufu kwa aupande wa wale walio katika
michezo.

Oscar
alipata ulemavu toka akiwa mdogo baada ya kufanyiwa upasuaji wa kukatwa
miguu yake.Alikatwa miguu akiwa na miezi kumi na mbili tu baada ya
kuzaliwa miguu yake ikiwa haipo sawa.
Post a Comment