Bahari ya Hindi (Picha ya liblary ) |
Jioni ya January 31 2013 millardayo.com iliripoti kuhusu kuzama kwa
Jahazi liitwalo Sunrise likitokea Tanga kulekea visiwani Zanzibar likiwa
na abiria 32 ambapo lilizama kwenye lile eneo la Nungwi .
Polisi Zanzibar walisema “tayari tumeshapokea watu 22 waliookolewa
wakiwa wazima na hakuna maiti iliyopatikana mpaka sasa hivi, waliokuwemo
kwenye chombo ni watu 32 hivyo watu bado watu 10 hawajulikani walipo”
Baada ya hapo millardayo.com iliahidiwa tena kuongea na Polisi baadae
ili kujua zoezi la uokoaji limefikia wapi, kweli Polisi walitoa tamko
lao usiku wakati AMPLIFAYA ya CLOUDS FM inamalizika.
Namkariri Kamanda akisema “Oparesheni imemalizika na hakuna yeyote
aliepatikana zaidi ya walewale 22 wa mwanzo ambao walipelekwa hospitali
na wote wamesharuhusiwa isipokua nahodha ambae bado amelazwa hospitali
kwa matibabu, kimsingi shauri linaendelea na upelelezi na baada ya
kukamilika sheria itachukua mkondo wake”
Kwa taarifa hiyo inamaana watu 10 ambao hawakuokolewa mwanzoni
wanahofiwa kufa maji manake mpaka oparesheni ya uokoaji imemalizika
hawakuonekana, kwa ushahidi unaweza kumsikiliza Kamanda wa polisi
akiongea hapo chini.
Chanzo: millardayo.com
إرسال تعليق