DR. Shein akihutubia wana CCM katika uzinduzi wa miaka 36 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduz |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shain amewatoa
mashaka WATU wanaohoji kutokuwepo kwa hati halisi ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar na kusema hati hiyo ipo na iwapo hawaamini
wanaweza kwenda Umoja wa Mataifa New York.
Dk Shein ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi wa sherehe za miaka 36 ya
Kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika kwenye viwanja vya Afisi
Kuu ya CCM Kisiwandu mjini Unguja.
Amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar chimbuko la kuasisiwa
kwake kulitokana na ridhaa ya wananchi wa pande mbili za Muungano na
kuwataka wanaowababisha wananchi kwa maneno ya mitaani kuacha kufanya
hivyo kwa sababu kila swali lao lina jawabu lake.
Dk Shein ambaye pia ni Makamo Mwenyeki wa CCM Zanzibar amesema
kuundwa kwa Muungano halikuwa ni jambo la kubahatisha bali lina malengo
yaliokusudiwa kabla ya kupatikana Uhuru ya Tanganyika mwaka 1961 na
kufanyika kwa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar Januri 12,1964.
Amesema wenye wasiwasi na kutokuwepo kwa hati ya Muungano wamfuate
ikulu awaonyeshe chumba walichokutana Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh
Abeid Karume na kufanya makubaliano ya mwisho kabla ya kuunganisha nchi
zao
Ameeleza kuwa madhumuni ya vyama vya TANU na ASP yalilingana tokea
vyama hivyo vikiwa katika harakati zake za kujikomboa hivyo kurahisisha
hata kazi ya kuziunganisha nchi hizo mwaka 1964 pia vyama hivyo na
kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977.
Aidha Makamo huyo Mwenyekiti wa CCM amewaeleza wananchi kuwa
Mapinduzi ya Zanzibar ndiyo Uhuru kamili wa visiwa vya Unguja na Pemba
huku akiwataka wananchi kutowasiliza watu wanaopotosha ukweli na
kuwataka kuacha kufanya hivyo.
Dk Shein amesema watu wanaobeza ukweli huo hawana nguvu ya hoja bali
wana lengo la kuwagawa wananchi ili waweze kuyafikia matarajio yao
ambayo amesisitiza yanapaswa kupuuzwa na kila mpenda amani na umoja.
Amewataka watu hao kupuuzwa kwasababu hawajui wafanyalo na kwamba
wanamangamanga ili kutaka kuwagawa wananchi bila ya kufikiri kwa makini .
Akizungumzia faida za Muungano Dk Shein amesema kiuhalisia wananchi
wa Zanzibar ndiyo wanaofaidika na Muungano huo kwani kila uendepa
katika Tamnzania Bara kuna wazanaziabri waliotamalaki na kuwekeza miradi
na mitaji .
Alisema Zanzibar inafaidika na siko la Bara ambapo kabla ya
Mapinduzi ilikuwa ikiagiza bidhaa za vyakula na mahitaji mengine kutoka
nchi za Pakistan, Japan na mashariki ya mbali jambo ambalo sasa
linapatikana kutoka Mikoa ya Bara
Kwa upnde wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai
akizunguimza kabla ya kumkaribisha Dk Shein ,amesema nguvu ya umoja na
maelewano kati ya visiwa vya Unguja na Pemba inatokana na kuwepo kwa
Muungano na kusema nje ya jambo hilo lolote linaweza kutokea.
Vuai amesema Muungano wa Tanzania licha ya kuleta tija za kiuchumi
lakini pia kwa kipindi chote cha miaka 49 ya kuwepo kwake umelinda na
kusimamia usalama wa raia na mali zao.
Amesema hata pale Tanznia ilipovamiwa na majeshi ya Idd Amini mwaka
1978,wanajeshi wa Zanzibar waliingia vitani ili kuihami nchi yao
vikiwemo visiwa vya Unguja na Pemba na kwamba nje ya Muungano umoja huo
unaweza kuparaganyika .
Naibu huyo Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,amesema CCM itaendelea
kujivunia matunda ya TANU na ASP kutokana na kupigania kwao maslahi ya
watu waliokuwa wakikandamizwa na kubaguliwa katika ardhi ya nchi zao.
Amesema vyama hivyo kwa pamoja vilihakikiisha vinajenga misingi
imara ya heshama na utu kwa kila binadamu na kuondosha matabaka,ubaguzi
wa rangi na maonevu hadi pale vilipoamua kuunganisha nguvu zake na
kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi mwaka 1977.
إرسال تعليق