SIKUWA NIMEIONA HII KAULI YA MBWANA SAMATTA BAADA YA KUIFUNGA CAMEROON.


.
Hii ni stori nzuri ambayo nimechelewa kuipata lakini nikaona kuna umuhimu wa kuiweka hapa na watu wangu waione.
Mwandishi wa habari Shaffih Dauda kupitia shaffihdauda.com aliripoti kwamba mchezaji Mbwana Samatta kasema anaamini goli la ushindi alilofunga dhidi ya Cameroon linatosha kumsafisha kwa mashabiki zake.
Hiyo imekuja baada ya mashabiki wa soka kuwazomea pamoja na Thomas Ulimwengu wakati Stars ikicheza na Zambia mwaka jana kwenye uwanja wa Taifa kutokana na kuchelewa kuripoti kambini kujiwinda na mchezo huo wa kirafiki.
Kitendo hicho kilimkasirisha kocha Kim Poulsen ambaye aligoma kuwapanga kwenye kikosi ambacho kilicheza na Tiafa Stars kuibuka na ushindi wa  1-0 likiwa ni goli la Mrisho Ngassa kwa shuti la mwendo mrefu.
Mbwana Samatta ambae nyumbani kwao ni Mbagala Dar es salaam amekaririwa akisema”naamini ushindi huu utakuwa umewafurahisha mashabiki na kurudisha imani kwetu, haikuwa lengo kuchelewa kujiunga na kambi, ni mambo tu yaliingiliana”

Post a Comment

أحدث أقدم