WAPINZANI WA SIMBA WATUA KIMYA KIMYA DAR, WAFIKIA HOTELI YA 'BEI CHAFU' MASAKI

Simba SC


Na Mahmoud Zubeiry
WAPINZANI wa Simba SC katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Recreativo de Libolo ya Angola wapo Dar es Salaam tangu jana na wamefikia katika hoteli ya Double Tree, Masaki.
Libolo wameingia Dar es Salaam bila kuwataarifu wenyeji wao, wakitokea moja kwa moja Ureno walipoweka kambi ya kujiandaa na mchezo huo wa kwanza utakaofanyika wiki ijayo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
LIbolo walituma watu wao mapema kuandaa mazingira ya timu yao kufikia na baada ya kukamilisha kila kitu, ndipo timu yao ikawasili hapa.
Tayari wamelipia Uwanja mzuri wa kufanyia mazoezi, Gymkhana katikati ya Jiji na hoteli ya Double Tree, pamoja na kujiandalia mazingira ya usafiri wakiwa hapa.
Wanaishi kwa tahadhari kubwa dhidi ya wenyeji, wakihofia eti kuhujumiwa na Wekundu hao wa Msimbazi.
Simba ipo mjini Arusha ambako leo itacheza mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya JKT Oljoro na baada ya hapo itaingia kambini rasmi kujiandaa na mchezo huo wa Afrika

Post a Comment

أحدث أقدم