TAZAMA PICHA ZA MWIGIZAJI MATUMAINI BAADA YA KUKIMBIZWA HOSPITALI GHAFLA


.
Siku ya Wapendanao february 14 imekua nzuri kwa watu wengine na mbaya kwa watu wengine, kwanza kabisa ni msiba wa msanii Goldie wa Nigeria ambae aliwahi kuiwakilisha nchi hiyo kwenye shindano la BBA 2012, pili ni model aliyeuwawa kwa risasi South Africa kwa kudaiwa kumfanyia mpenzi wake suprise lakini mpenzi wake akajua ni jambazi, tatu ni mwigizaji Mtanzania Matumaini kukimbizwa hospitali ghafla baada ya kuzidiwa.
Matumaini ambae anameza dawa 15 kila siku kutokana na matatizo ya miguu kuwaka moto, ini pamoja na figo kumsumbua.. alipewa na Meya wa Ilala Jerry Silaa msaada wa gari la wagonjwa lililotumwa mpaka kwao Vingunguti kwenda kumchukua baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi.
Kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Mnazi mmoja Dar es salaam ambapo mpaka jioni ya february 14 hali yake haikua nzuri, amekua akiishi Msumbiji kwa miaka mitatu baada ya kuolewa na raia wa nchi hiyo, alikwenda huko kutafuta maisha baada ya kufanya uamuzi wa kwenda kuuza kopi zake 300 za movie yake ya Comedy.
.
.
.
Baadhi ya waigizaji wa movie Tanzania waliojitokeza kwenda kumjulia hali.

Post a Comment

Previous Post Next Post