Uganda yawania nafasi ya urais Mkutano Mkuu Umoja wa Mataifa

Uganda yawania nafasi ya urais Mkutano Mkuu Umoja wa Mataifa. imewakilisha katika Umoja wa Afrika (AU) ugombea wake kwa nafasi ya urais wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), nafasi ambayo iwapo itapatikana itasaidia ushawishi mkubwa katika anga za kimataifa.
Katika kuwasilisha huko Uganda itakabiliana na maombi kama hayo kutoka Camoroon ambayo pia imeonyesha nia ya kuwania kiti hicho kwa kikao cha  69 ambacho kitaendeshwa kutoka 2014 hadi 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda  Sam Kutesa (pichani) amesisitiza kuwa sasa ni wakati wa Afrika kushika wadhfa huo, tena zaidi Afrika Mashariki.
Amesema mabara kadhaa yameshika wadhfa huo ikiwemo na sehemu nyingine za Afrika isipokuwa Afrika Mashariki ambayo ilishika mwaka 1979.
Iwapo Uganda itafanikiwa, amesema itatumia nafasi yake hiyo kusukuma mbale suala la kuwemo na nchi ya Afrika katika Baraza La Usalama la Umoja wa Mataifa.

Post a Comment

أحدث أقدم