WAZIRI MKUU AUNDA TUME KUCHUNGUZA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE

                                                              
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
WAZIRI
 MKUU Mizengo Pinda ameunda Tume maalum itakayofanya uchunguzi wa 
matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa na Waziri wa 
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa Februari 18, mwaka huu.
 
Katika
 matokeo hayo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi
 waliofanya mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli. 
 
Katibu
 Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Peniel Lyimo amesema Tume hiyo ambayo 
inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo inajumuisha wadau 
kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania Association
 of Managers and Owners of Non-Government Schools/Colleges (TAMONGSCO), 
Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 
na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia masuala ya elimu.
 
 
Wadau wengine watatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati
 ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari 
Tanzania (TAHOSSA).
 
Amesema Serikali inawaomba wadau wa elimu, 
wazazi, walezi na wananchi wote kwa ujumla watoe ushirikiano kwa Tume 
ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi.
 
(mwisho)
 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021, 
DAR ES SALAAM.
JUMAMOSI, FEBRUARI 23, 2013.
 

Irene K. Bwire,
Email: irenekaki@yahoo.com
"The secret to success is constancy to purpose"

Post a Comment

أحدث أقدم