Wachezaji
26 wa timu ya Young Africans wanaingia kambini leo jioni katika hosteli
zilizopo makao makuu ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwani tayari kwa
maandalizi ya mchezo wa ligi Kuu ya Vodacom siku ya jumatano dhidi ya
timu ya African Lyon katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es
sHaruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Hamis Kiiza walisharejea tangu siku ya
ijumaa tayari kabisa kuungana na wachezaji wenzao na leo jioni
wataingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo dhidi ya African
Lyon siku ya jumatano.
Katika
mchezo huo wa jumatano Young Africans inahitaji ushindi ili kuendelea
kuongoza msimamo wa Ligi Kuu kisha kuweka mazingira mazuri ya ushindi
katika mchezo utakaofuata dhidi ya Azam Fc februari 23, 2013 katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
alaam.
Young
Africans ambayo inaongoza msimamo wa ligi kuu ya Vodacom (VPL) kwa kuwa
na pointi 33 huku ikiwa imecheza michezo 15, inafuatiwa nafasi ya pili
na timu ya Azam FC yenye pointi 30 ambayo leo inacheza dhidi ya Mtibwa
Sugar ya Morogoro katika uwanja wa Manungu Complex.
Wachezaji
wote walikuwa wamepewa mapumziko ya siku mbili kwa siku za jumamosi na
jumapili kabla ya leo jioni kuingia kambini na kesho asubuhi kuanza
mazoezi ya pamoja katika uwanja wa mabatini Kijitonyama.
Ikumbukwe
Young Africans ilitoa wachezaji 8 kwa ajili ya kujiunga na timu zao za
Taifa kwa ajili ya michezo ya kirafiki ya kalenda ya FIFA lakini
wachezaji 18 waliobakia walikua wakiendelea na mazoezi kila siku asubuhi
mpaka wachezaji wengine waliporejea na kuendelea na mazoezi kwa pamoja.
Didier
Kavumbagu ana nafasi ya kuongeza idadi ya mabao katika mchezo wa
jumatano kufuatia kurudi katika hali nzuri ya kimchezo, huku Jerson
Tegete, Hamis Kiiza na Said Bahanuzi nao wakiwa na nafasi ya kuongeza
mabao katika mchezo huo.
إرسال تعليق