
Video hii inapatika youtube ikiwa na maneno haya
Kwa muda sasa hapa tanzania kumekuwepo na matukio ya
kusikitisha ya kuteka na kutesa wanaharakati wa haki za binadamu akina
mwangosi, ulimboka na wengine.. sisi wazalendo na wapenda amani ya tanzania
tunasema tumechoka na sasa basi tunaweka wazi kila kitu ili umma ujue
kinachoendelea..kweli daima itakuweka huru...video hii inaonyesha sehemu tu ya
matukio yaliyokwishatekelezwa na chadema , mpango mzima ukiratibiwa na
mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama willifred lwakatare kwa maelekezo ya
mwenyekiti mh. mbowe na katibu mkuu dr slaa. katika video hii lwakatare anatoa
maelekezo kwa kijana wake kwenda kutekeleza utekaji wa mwandishi wa kampuni ya
mwananchi huku akitolea mfano wa matukio ambayo chama kiliyatekeleza kama lile
la igunga ambapo mussa tesha alimwagiwa tindikali na lile la morogoro ambapo
kijana mmoja alifariki katika vurugu za maandamano ya chadema ambapo polisi
walitoa taarifa kuwa kijana huyo ameangukiwa na kitu kizito. hii video ni
sehemu tu ya video zingine ambazo tutazitoa wakati muafaka ukifika..
إرسال تعليق