
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile
Watu
watatu wamefariki dunia mkoani Morogoro katika matukio tofauti akiwemo
mama aliyeuawa na mwanaye na watoto wawili kuliwa na mamba.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema katika tukio
lililotokea Machi 14, mwaka huu, majira ya jioni huko Chamwino Manispaa
ya Morogoro, mwanamke mmoja Dorcas Lugano (55) aliuawa kwa kupigwa shoka
ubavuni baada ya kumtaka mwanaye akatafute kazi ili aanze kujitegemea
baada ya umri kuwa mkubwa.
Awali mwandishi wa
habari hizi alifika eneo la tukio na kushuhudia umati mkubwa wa watu
waliofika eneo hilo kushuhudia mauaji hayo, ambapo baadhi ya waliohojiwa
walidai kabla ya tukio hilo, kuliibuka ugomvi baina ya mwanamke huyo na
mwanaye, Frank Hilari, ambapo mama huyo alitoka mbio na kukimbilia
nyumba ya jirani.
Hata hivyo
mashuhuda hao ambao walikataa majina yao kutajwa, walidai baada ya hali
hiyo, mtoto huyo, alimfuata nyuma mama yake na kuingia katika nyumba
hiyo iliyokuwa na mwanamke mmoja mzee, ambaye alishindwa kuamulia na
kumpiga shoka mama yake, na kusababisha kifo chake.
Kufuatia hali hiyo,
baadhi ya watu walimdhibiti asiendelee na madhara kwa watu wengine
waliokuwa jirani, kwa kumfungia ndani hadi pale polisi walipofika na
kumchukua kumpeleka kituo cha polisi.
Kamanda Shilogile,
alikiri kuwa mtuhumiwa amekamatwa na polisi na inasadikiwa kuwa kijana
huyo ana matatizo ya akili lakini uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado
unaendelea ili aweze kufikishwa mahakamani.
Akizungumzia
matukio mengine, Kamanda huyo wa Polisi alisema Machi 13, mwaka huu,
majira ya saa 10 jioni huko Vigolegole kata ya Bwakila wilaya ya
Morogoro, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mngazi Cosmas Bernad ( 8)
alikutwa amefariki dunia baada ya kuliwa na mamba.
Alisema kuwa mtoto
huyo alichukuliwa na mamba siku tatu kabla ya kifo chake, wakati akinawa
katika maji ya moto Mgeta hadi Machi 13 mabaki ya mwili wake
yalipoonekana katika mto huo.
Wakati huo huo,
mtoto mwenye umri wa miaka sita, Sikudhani Juma, aliliwa na mamba wakati
akiogelea na wenzake katika Mto Ngerengere na hadi sasa maiti yake
haijaweza kupatikana.
Shilogile alisema tukio hilo lilitokea Machi 12, mwaka huu, majira ya saa 11 jioni huko Ngerengere katika wilaya ya Morogoro.
Aidha Ibrahim
Jaribu mkazi wa eneo la Sia Ujenzi katika kata ya kiwanja cha Ndege
manispaa ya Morogoro anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwachoma moto
midomo watoto wake wawili Malik Jaribu(5) na Ibarahim Jaribu (10) wote
wanafunzi wa Shule ya Msingi Msavu B baada ya kula karanga zake za
biashara.
Imedaiwa baba huyo aliwachoma moto
midomo watoto hao Machi 13, mwaka huu saa 9.45 jioni baada ya watoto hao
kushinda na njaa siku nzima na kuamua kula karanga hizo.
إرسال تعليق