Na Gustav Chahe, Iringa
MTU mmoja amenusurika katika ajali baada ya gari
alilokuwa akisafiria kuacha njia na kutumbukia kwenye mtaro wa maji.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 11 alfajiri katika
barabara ya Iringa – Dodoma maeneo ya Sabasaba katika Manispaa ya Iringa ambapo
gari lenye namba za usajili T 287 AAG Prado limetumbukia kwenye mtaro kwa kile
kilichoelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu katika maungio ya tairi
(boll joint).
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na kikosi cha
uokoaji (K.B. WORKSHOP) zinasema kuwa baada ya kupata hitilafu katika tairi
moja, gari lilipoteza mwelekeo na kuhama njia kasha kutumbukia kwenye mtaro.
Imeelezwa kuwa katika gari hilo alikuwemo dereva
pekee ambapo hata hivyo hakupata majeraha makubwa.
Gari hilo lilikuwa likitokea mjini Iringa kuelekea
Kihesa ambapo mara baada ya ajali hiyo imeelezwa kuwa dereva alikwenda
kupumzika kutokana na maumivu ya majeraha aliyopata japo kuwa jina lake
halikutajwa.
Mtandao
huu umeshuhudia gari lenye namba za usajili T 332 AKP mali ya K.B.WORKSHOP
wakiokoa gari hilo lililokuwa kwenye mtaro.
إرسال تعليق