UHURU KUDONDOSHA MASTAR KENYA

Uhuru Kenyatta
Taarifa zisizokuwa rasmi zime premier all over East Africa kwasasa kuwa huenda timu teule ya taasisi ya rais mteule Uhuru Kenyatta inashughulikia orodha ya wasanii watakaofanya onyesho kubwa huko kenya siku ya kuapishwa kwake.
Mtandao mmoja maarufu nchini kenya umenasa na kuvujisha majina ya ma-star wakali kibao akiwemo Rihanna, Chris Brown, Nicki Minaj, Toni Braxton, Alaine, Burning Spears na kudai kuwa mastar hao watafanya yao wakati ambapo Uhuru Kenyata atakuwa anafanya yake katika siku ya kuapishwa.

Uvumi huo usio na kichwa wala miguu umewashika wengi maskio hasa wapenzi wa burudani huko Kenya licha ya kutokuwa na uthibitisho wowote kuhusu jambo hilo.
Tetesi zimevuma kila kona siku ya jana kuwa kwasasa maandalizi ya onyesho hili kubwa kabisa Kenya yapo katika hatua za mwisho info rasmi zikiwa mbioni kutangazwa soon kwenye vyombo vya habari.

Post a Comment

أحدث أقدم