| Kushoto ni kijana ambaye jina halikutambuliwa mara moja akipigwa na polisi. |
| Kijana ambaye hana shati akichapwa na polisi aliye mbele yake. |
| Nyuma ya pikipiki ni jana anayeendelea kupigwa na polisi baada ya kuteguliwa mguu na kupasuliwa usoni huku mkono wake ukiwa umechubuka. |
===========================================
Na Gustav Chahe, Dodoma
Na Gustav Chahe, Dodoma
Ni nje kidogo na stendi ya daladala ziendazo Chuo cha
Pipango na Nanenane, Polisi walipomkamata kijana mmoja ambaye jina lake
halikutambuliwa mara moja mbele yangu na kuanza kumpiga.
Wakati wanaendelea kumpa kichapo, wananchi walitaka
kujua kosa la huyo kijana ni nini ndipo alipojitokeza askari mmoja na kusema ni
mlevi.
Wakati hayo yakiendelea nikashuhudia kwa macho yangu
askati aliyekua amevaa mavazi ya kiraia akiwa na boriti na kuanza kumpiga kijana
huyo miguuni, mgongoni hata mikononi na kumpasua usoni na kumtegua
mguu.
Hali hiyo ilinisukuma kuchomoa kamera katika mkoba
wangu na kuanza kupoga picha kwa kiicho japo watu walikuwa wengi iawa ni shida
kupata picha lakini nilijitahidi kupata picha Fulani.
Nikaona haitoshi nikaamua kumsogelea askari mmoja na
kunza kumuuliza ni kosa gain kijana amelikosa kiasi cha kuchapwa kama
mnyama.
Wakati nikiuliza hivyo askari huyo akwaita wenzake na
kusema huyu ni mwandishi anatafuta nini hapa.
Kibao kilinigeukia nikaoneshwa bunduki ndipo
nilipofanikiwa kujichanganya na watu nikakimbia na ananchi wasamaria wema
wakaamua kunificha.
Zilisikika sauti za wananchi wakisema “mlindeni
mwandishi huyo ili akafikishe hayo kwa taifa zima ili watu waone unyama
wanaotufanyia polisi”.
Muda mfupi walitokea askari wa kikosi cha kutuliza
ghasia na kufukuza wananchi kwa kuwatishia bunduki jambo lililowasononesha watu
kuwa hawana uhuru.
“Akionekana mtu hapa tunamuwasha. Ondokeni hapa mara
moja hatuwataki hapa. Jitieni na kimbelembele chenu muone. Potea” alisema
askari.
Wakati hayo yakitendeka ikatokea gari ya polisi na
kumtupia yule kijana na kuondoka naye huku akiendelea kupigwa kwenye ndani ya
gari wakati anapelekwa kituoni.
Post a Comment