Naibu spika Mh. Job Ndugai amempa siku
saba kuanzia leo mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kutoa
uthibitisho wa kauli aliyoitoa bungeni hii leo kuwa rais jakaya Kikwete
ni kinara wa ugaidi hapa nchini
Naibu spika amempa
mh. Lema muda huo kufuatia mvutano mkali ulioibuka bungeni wakati
akichangia hoja hii leo bungeni Dodoma katika awamu ya pili ya saa 11
jioni
Kufuatia ushauri uliotolewa na
Mwanasheria mkuu wa serikali kuwa kauli hiyo iliyotolewa na Lema ni ya
kumdhihaki rais, hivyo anatakiwa kuifuta jambo lililokataliwa na Mh.
Lema
Kabla
ya mh Naibu spika kutoa uamuzi huo mbunge Lema alikubali kuthibitisha
kauli yake hiyo ndipo alipopewa siku saba kuanzia leo
إرسال تعليق