JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
TAMKO LA SERIKALI KUHUSU UHAMAJI KUTOKA MFUMO WA
UTANGAZAJI WA ANALOJIA KWENDA DIJITALI
Mabadiliko katika mfumo wa utangazaji kutoka mfumo wa analojiakwenda
katika mfumo wa dijitali ni utaratibu ambao unaendeleaulimwenguni kote.
Mabadiliko haya yanatokana na makubaliano ya nchiwanachama wa Shirika la
Umoja wa Mataifa lenye dhamana ya masualaya mawasiliano yaani
International Telecommucations Union
yaliyofanyika mwaka 2005 huko Geneva, Uswisi. Makubaliano ya
nchiwanachama ni kuzima kabisa matangazo katika mfumo wa analojia
nakutumia mfumo wa utangazaji wa dijitali ifikapo tarehe 17 Juni
2015.Ili kuhakikisha mabadiliko haya yanafanyika kwa ufanisi, tija na
piakutoa muda wa kutosha wa kutekeleza mabadiliko haya, mwaka
2005Serikali ilianza mchakato wa uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji
waanalojia kwenda dijitali ambao ulihusisha wadau wote, wakiwemowamiliki
wa vyombo vya habari na vituo vya utangazaji wa televisheni,hatua kwa
hatua, hadi kuridhia ratiba nzima ya uzimaji wa mitambo yaanalojia. Kwa
kifupi mchakato wa uhamaji ulipitia hatua zifuatazo:
Mwaka 2005
:Waraka wa kwanza wa mashauriano (consultativedocument) kuhusu umuhimu
na faida za kuhama kutokamfumo wa utangazaji wa analojia kwenda
dijitaliulitayarishwa na kusambazwa kwa wadau wote;
Mwaka 2006:
Waraka wa pili wa mashauriano na mapendekezo yamuundo wa leseni kwenye
mfumo wa utangazaji wateknolojia ya dijitali ulitayarishwa na kusambazwa
kwawadau wote;
Mwaka 2007:
Kamati ya kiufundi inayoshughulikia uhamaji kutokamfumo wa utangazaji wa analojia kwenda dijitaliiliundwa;
1
Mwaka 2007:
Mkutano mkuu uliojumuisha vituo vyote vya utangazajinchini ulifanyika
Bagamoyo kupitisha maazimio yamfumo wa leseni za utangazaji utakaotumika
kwenyemfumo wa dijitali;
Mwaka 2010:
Kampuni tatu (3) zilipewa
leseni za ujenzi wamiundombinu ya utangazaji ya dijitali. Kampuni
tatuzilizopewa leseni za kusambaza matangazo ya dijitali niAgape
Associates Limited, Basic Transmission Limited,na Star Media (T)
Limited. Kampuni hizo zilipewa lesenibaada ya kuthibitisha kuwa zina
uwezo wa kujengamiundombinu ya kurushia matangazo katika mfumo
wadijitali;
Mwaka 2010
:Kamati ya Kitaifa ya Kuratibu Mabadiliko
ya Utangazajitoka mfumo wa analojia kwenda dijitali iliundwa.Kamati hii
hukutana kila baada ya miezi mitatukutathmini maendeleo ya ubadilishaji
wa mfumo wautangazaji;
Mwaka 2011
:Kampeni ya Kitaifa ya
kuelimisha umma kuhusumabadiliko ya mfumo wa utangazaji ilizinduliwa
rasmina Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania.Ili
kuhakikisha kuwa ujenzi wa miundombinu ya urushaji wa matangazokatika
mfumo wa dijitali unaendana na ratiba ya uhamiaji katikamfumo wa
matangazo kutoka mfumo wa analojia kwenda dijitali,taarifa za mara kwa
mara zimekuwa zikiletwa na wajenzi wamiundombinu hiyo katika Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania nakujadiliwa na Kamati mbalimbali zinazohusiana na
masuala ya uhamajikatika mfumo wa utangazaji wa dijitali. Taarifa hizo
zimekuwazikionyesha kuwa ujenzi wa miundombinu unaendelea vizuri
nakwamba ratiba ya uzimaji wa mitambo ya analojia nchini itakwendakama
ilivyokubalika na wadau wa utangazaji.Kufuatia uzinduzi wa Kampeni ya
Kitaifa ya Kuelimisha umma kuhusumabadiliko ya mfumo wa utangazaji
kutoka katika mfumo wa analojiana kwenda katika mfumo wa dijitali
uliofanywa na Mhe. Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali, kwa
kupitia Mamlaka yaMawasiliano Tanzania, iliandaa
Mkakati Maalum wa Mawasiliano
ambao ulilenga katika kuhamasisha wananchi kuhusu uhamaji katikamfumo
wa utangazaji wa dijitali. Njia mbalimbali zimetumika katikakuelimisha
umma kuhusu mabadiliko ya mfumo wa utangazaji ikiwa nipamoja na kufanya
mikutano ya hadhara sehemu mbalimbali, kutoa
2
vipeperushi
na matangazo katika magazeti, redio na televisheni,kufanya majadiliano
katika televisheni na redio ambayo yalihusisha piamaswali kutoka kwa
wadau mbalimbali, kuweka taarifa katika tovutikuhusu masuala mbalimbali
ya uhamaji katika mfumo wa utangazaji.Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa
uhamasishaji na elimu kwa ummaimetolewa kwa kiasi kikubwa na wananchi
wamehamasika sana katikakuingia katika mfumo wa utangazaji wa dijitali
kutoka ule wa analojia.Hii ni kutokana na wananchi wengi kujitokeza
kununua ving’amuzi(visimbuzi) kwa wingi katika Jiji la Dar es Salaam na
maeneo mengineambayo matangazo katika mfumo wa analojia yalitarajiwa
kuzimwa.Aidha,
hapakuwa na mapendekezo yoyote kutoka kwa wajenzi wamiundombinu ya urushaji wa matangazo ya dijitali
kuwawatashindwa kujenga miundombinu hiyo kwa wakati ifikapo tarehe
31Desemba 2012, siku ambayo ilikuwa imekubalika kuzima mitambo
yautangazaji ya mfumo wa analojia na kuanza kutumia mfumo wadijitali.
Tarehe 31 Desemba 2012, Serikali ilianza kuzima matangazohayo kwa awamu
ili kubaini na kushughulikia changamoto mbalimbaliambazo zingeweza
kujitokeza katika mabadiliko hayo.Uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa
analojia kwenda katika mfumowa utangazaji wa dijitali ilianza
kutekelezwa tarehe 31 Desemba 2012kwa kuzima mitambo 14 ya televisheni
inayotumia utangazaji wamfumo wa analojia katika jiji la Dar es Salaam
ambapo wananchi wengiwalinunua ving’amuzi ili waweze kujiunga na mfumo
mpya wautangazaji wa dijitali. Kadhalika, uzimaji wa mitambo ya
analojiakwenye miji ya Dodoma na Tanga ulifanyika tarehe 31 Januari
2013.Uzimaji wa mitambo ya analojia kwa jiji la Mwanza ulifanyika
tarehe28 Februari 2013. Uzimaji wa mitambo kwa miji ya Arusha na
Moshiumefanywa tarehe 31 Machi 2013. Kwa ujumla wananchi
wamekuwawakijitokeza kwa wingi kujiunga na mfumo huu mpya wa utangazaji
nahakuna matatizo yaliyojitokeza zaidi ya changamoto kadhaa
ambazozimeendelea kupatiwa ufumbuzi.Ikumbukwe kuwa uzimaji wa urushaji
wa matangazo katika mfumo waanalojia na kuanza kutumika kwa mfumo wa
dijitali umefanywa mahaliambapo kuna mawimbi (signal) ya televisheni ya
dijitali tu. Paleambapo hakuna mawimbi ya televisheni ya dijitali,
matangazo yatelevisheni yameendelea kurushwa katika mfumo wa analojia
hadiwakati ambapo mawimbi ya televisheni ya dijitali yatakapofikia
mahali
3
Post a Comment