Dk.
 Mwele Malekela ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR akifungua Mjadala juu 
ya Utafiti wa udhibiti wa ugonjwa wa mabusha na matende kwa nchi za 
Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika. 
 | 
Na Mroki Mroki wa Father Kidevu Blog Arusha
Wilaya
 94 zimefikiwa katika zoezi la unyweshaji dawa za Matende na Mabusha  na
 utoaji elimu linaloendeshwa chini ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti 
magonjwa yasiyopea kipaumbele (NTD) unaoratibiwa na Wizara ya Afya na 
Ustawi wa Jamii.
Mkurugenzi
 Mkuu wa NIMR Dakta Mwelecele Malecela ameyasema hayo mjini Arusha 
wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika Kongamano la 27 la 
taasisi hiyo la  Sayansi la Kongamano la Pili la Afya Moja Afrika 
 linaloendelea mjini humo.
Dk.
 Malecela amesema watu milioni 14 wamenufaika na huduma ya matibabu ya 
mabusha na matende  katika wilaya hizo 94 ambazo zimefikiwa katika zoezi
 la ugawaji dawa na tiba.
Aidha
 alieleza kuwa katika wilaya ya pangani jumla ya watu mia mbili 
waliokuwa wanasumbuliwa na mabusha wamepatiwa tiba kwa njia ya upasuaji 
na tayari wamerejea katika hali ya kawaida na kuweza kuendelea na 
shughuli za maendeleo ya jamii yao.
Dk. 
Malecela amesema Programu ya kudhibiti Metende na Mabusha imeandaa 
mkakati maalum wa elimu kwa umma utakaowawezesha watanzania kupata elimu
 na mbinu za kuwawezesha kushiriki harakati za kitaifa za kutokomeza 
magonjwa hayo nchini ambayo yameleta hofu na mashaka katika jamii 
kufuatia imani potofu.
Mkurugenzi
 Mkuu huyo wa NIMR ameitaka jamii kushiriki katika zoezi la unyweshaji 
dawa kwa miaka mitano mfululizo bila kuchoka ili kuweza kumaliza dozi na
 hiyvo kuweza kujikinga na maambukizi na hatimaye kutokomeza magonjwa 
hayo.
Dk.
 Malecela amesema Wilaya ya Tandahimba, mkoani Lindi imefanikiwa 
 kupunguza wagonjwa wa matende na mabusha na kufikia kiwango cha chini 
ya asilimia moja kutokana na  jitihada za pamoja zinazoendelea za 
kutokomeza magonjwa hayo chini ya Mpango wa Taifa wa Kutokomeza magonjwa
 yasiyopewa Kipaumbele.
Pamoja mbu wa malaria aina ya Anopheles, ugonjwa wa Matende na mabusha pia huambukizwa kwa na mbu aina ya  Culex. 
Magonjwa
 haya  pia husababishwa na minyoo inayoishi kwenye damu na maji damu 
ambayo husababisha madhara makubwa kwenye miguu ,matiti, mikono na 
makende.
Mbu
 aina ya Anopholes huweka mazalia yake katika maji yaliyotuama ambapo 
Culex huweka mazalia yake katika maji machafu yakiwwemo yale katika 
mashimo ya choo na madimbwi.
Aidha
 Dk.Mwele amesema kuwa serikali imefanya jitihada kubwa sana kwani mfuko
 wa rais wa kupambana na matende na mabusha umeonyesha mafanikio makubwa
 na kuwezesha watu kupata matibabu kwa njia ya upasuaji.
Wagonjwa
 480 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mabusha katika mkoa wa Lindi 
katika mwa huu, ambapo wagonjwa 54 kati yao wamekwishafanyiwa upasuaji 
huo Mwezi April mwaka huu.
Baadhi ya washiriki ambao ni watafiti wakifuatilia mada za mjadala huo.
Dk.
 Upendo Mwingira akitoa mada yake juu ya matumaini ya kutokomeza Ugonjwa
 wa Matende na Mabusha hasa kufuatia utafiti wake Wilayani Tandahimba.
Mmoja wa watafiti
Sehemu ya washiriki wakifuatilia majidiliano hayo juu ya ugonjwa wa matende na Mabusha.
Watoa mada mbali mbali kutoka nchi za Afrika wakitoa mada zao juu ya Tathmini ya ugonjwa wa Mabusha na Matende katika nchi zao.
إرسال تعليق