
JESHI la
Polisi Mkoa wa Kinondoni linamshikilia Ahmad Mohamed Sharif (38),
mfanyabiashara na mkazi wa Mwananyamala Msisiri ’A’ kwa tuhuma za
kuwaingilia kinyume cha maumbile wanafunzi wanne wa darasa la nne wa
Shule ya Msingi Misisiri ’A’.
Ahmad
amekuwa akiwaingilia kinyume cha maumbile wanafunzi hao katika kipindi
cha mwezi Aprili na Mei mwaka huu kwa nyakati tofauti.
Kati
ya wanafunzi hao, wawili wana umri wa miaka 10 na wengine wawili wana
umri wa miaka 12 na 11 wote wakiwa ni wanafunzi wa Misisiri A.Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo, Suzana Orege (35) alisema wanafunzi hao wamekuwa na
mahudhurio mabaya shuleni kwa zaidi ya mwezi mmoja na ndipo walipojaribu
kuwafuatilia kwa karibu ili kubaini sababu za wanafunzi hao
kutohudhuria shuleni.
Suzan
alisema ilipofika Mei 9, mwaka huu walifanikiwa kuwapata wanafunzi
watatu (majina yanahifadhiwa) lakini mmoja alikimbia kusikojulikana na
walipowahoji sababu za wao kutohudhuria masomo, waliwaeleza kuwa huwa
wanatoka nyumbani kama kawaida kwa ajili ya kwenda shule, lakini huishia
nyumbani kwa Ahmed.
Alisema
walipohojiwa zaidi walisema baada ya kufika nyumbani kwake huwawekea CD
za ngono na kisha kuwaingilia kinyume cha maumbile na kuwapa maandazi,
chapati, bagia, biskuti na kuwatishia wasiseme kwa mtu yeyote na endapo
watasema atawafanyia kitu kibaya .
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Charles
Kenyela amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, ambapo alisema
alikamatwa Mei 10, mwaka huu na atafikishwa mahakamani kesho.
Kamanda ametoa onyo kwa watu wengine wenye tabia chafu kama hiyo kuacha mara moja kabla ya kukumbwa na mkono wa sheria.
إرسال تعليق