MBUNGE wa Jimbo la Hai, Mheshimiwa Freeman Mbowe (pembeni mlangoni
kulia) akishuhudia kile alichokiita ni 'maajabu ya elimu ya Tanzania'
pale alipokuta wanafunzi wa darasa la tatu (kushoto) na darasa la nne
(kulia) katika Shule ya Msingi Mlima Shabaha, wakifundishwa ndani ya
chumba kimoja cha darasa kwa wakati mmoja, wakisoma masomo tofauti,
wakisimamiwa na walimu wawili tofauti.
Wakati wanafunzi wa darasa la tatu walikuwa wanafundishwa somo la hesabu, wale wa darasa la nne walikuwa wakisoma somo la lugha ya Kiingereza. Katikati ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Stephano Ndosi, kushoto ni Mwalimu Anameni Kimaro na kulia ni Mwalimu Love Hoza.
Wakati wanafunzi wa darasa la tatu walikuwa wanafundishwa somo la hesabu, wale wa darasa la nne walikuwa wakisoma somo la lugha ya Kiingereza. Katikati ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Stephano Ndosi, kushoto ni Mwalimu Anameni Kimaro na kulia ni Mwalimu Love Hoza.
Mbowe aliwaambia walimu na wazazi wa watoto wanaosoma shule hiyo kuwa
hali hiyo haikubaliki na akawaahidi kuwa atashirikiana nao kuhakikisha
kuwa ndani ya wiki moja watoto hao wanaondokana nayo ili wasome katika
mazingira sahihi waweze kujifunza, kupata maarifa, taarifa, kuelewa na
kufaulu.
Wazazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo walimwambia mbunge huyo
namna ambavyo wamehangaika kwenda sehemu mbalimbali, ikiwemo kumuona
Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya ya Hai, kwa ajili ya kutatuliwa tatizo
katika shule yao, lakini waliambulia patupu.
Walihoji juu ya utaratibu wa kusimamia elimu nchini, hasa ngazi ya
msingi hadi sekondari, ambapo kumekuwa na mkanganyiko mkubwa kutokana na
kuwekwa chini ya wizara mbili tofauti, huku wakienda mbali na kuhoji
zaidi kwa nini mgao wa bajeti unaohusika na kuwasaidia wananchi katika
ujenzi wa madarasa na masuala mengine, umekuwa ukichelewa kufika katika
halmashauri za wilaya, kupitia TAMISEMI.
Baada ya ziara ndogo kuzungukia maeneo ya shule hiyo iliyofuatiwa na
kikao kifupi kilichofanyika shuleni hapo, ambapo Mwalimu Mkuu, Ndosi,
Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi wa shule hiyo, Noeli Elia, Mwenyekiti wa
Mtaa wa Kilima Shabaha, Emmanuel Leiza kutoa taarifa juu ya hali ya
shule hiyo, Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,
aliomba kuondoka na Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi na Mwenyekiti wa
Serikali ya Mtaa, kwa ajili ya kikao ofisini kwa mbunge, ambako
aliidhinisha wapate milioni 6.5 kwa ajili ya kukamilisha mahitaji ya
vifaa/mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa ajilinya wanafunzi na
waalimu katika shule hiyo.
Chadema blog
Post a Comment