Wachezaji
na viongozi wa Yanga wakishangilia ubingwa kwa kufungua na kuripua
Champagn, baada ya kukabidhiwa Kombela lao la Ubingwa wa Ligi Kuu ya
Tanzania Barailiyomalizika leo, ambapo Yanga imeshangilia ubingwa wake
kwa kumfunga mtani wake wa Jadi Simba, mabao 2-0, katika mchezo
uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao
ya Yanga, yalifungwa na Didier Kavumbagu, aliyeunganisha mpira kwa
kichwa Kona iliyopigwa na Haruna Niyonzima, kipindi cha kwanza na Hamis
Kiiza, kipindi cha pili, aliyeunganisha mpira uliorushwa na Mbuyu Twite.
Simba walipoteza penati yao iliyopigwa na Mussa Mudde, waliyoipata
kipindi cha kwanza baada ya Canavaro kumuangusha Ngasa katika eneo la
hatari, na kufanya timu hizo zina kwenda mapumziko Yanga ikiwa mbele kwa
bao 1-0.
Wachezaji wakindellea kushangilia ubingwa wao....
Katika
tukio jingine ni pale mashabiki wa Yanga, walipomvizia Ngasa baada tu
ya kushuka katika jukwaa alipopanda kupokea Nishani yake na timu yake
iliyopanda kupokea zawadi ya mshindi wa tatu, walimvamia na kumteka na
kisha kumvisha Jezi ya Yanga na kumbeba juu juu na kuanza kuzunguka naye
pembezoni mwa Mashabiki wa Yanga huku wakipiga kelele za kushangilia,
hadi walipotokomea naye nje ya mageti ya kutokea uwanjani humo.
Post a Comment