
Na Goodluck Eliona, Mwananchi
KWA UFUPI
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa baada ya wazazi kubanwa na Serikali wanapowaachisha mabinti zao shule kwa lengo la kuolewa, wengine wamebuni mbinu za kusingizia vifo kwa mabinti hao.
Mkuranga. Wazazi wilayani hapa wamebuni mbinu mpya ya kuwaachisha shule watoto wa kike, ambapo wanashirikiana na baadhi ya walimu kuandika ripoti za uongo kwamba mabinti hao wamefariki dunia.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa baada ya wazazi kubanwa na Serikali wanapowaachisha mabinti zao shule kwa lengo la kuolewa, wengine wamebuni mbinu za kusingizia vifo kwa mabinti hao.
Kwa mujibu wa uchunguzi gazeti hili kuna idadi kubwa ya wanafunzi wa kike katika shule za sekondari na msingi, ambao wameacha shule baada ya kupata ujauzito na wengine kuolewa.
Taarifa za uchunguzi zilibaini katika shule za sekondari za Kizomla na Mgulani zaidi ya wanafunzi ishirini (majina tunayo) walipata ujauzito na watano waliolewa kati ya mwaka 2009 na 2012.
Akizungumzia utoro na upungufu wa wanafunzi shuleni hapo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Frank Mjenga alisema kuwa wanafunzi wanazidi kupungua kutokana na utoro, kupata mimba pamoja na kukosekana kwa mazingira rafiki kwa wanafunzi.
“Hawa wanafunzi wanapungua kwasababu ya uzembe…kwa mfano mwaka huu nimepewa wanafunzi 18 tu, darasa linatakiwa kuwa na wanafunzi 40,” alisema Mjenga.
Mkazi wa kijiji cha Mgulani, Jafari Jongo alisema kuwa kuna wazazi ambao wanashirikiana na walimu kuwatorosha wanafunzi na kuwaoza kwa kutumia njia mbalimbali kuficha ukweli.
“Imetokea mara mbili hapa katika Shule ya Msingi Mgulani, wazazi walishirikiana na walimu kuwaozesha wanafunzi halafu wakaandika kuwa wanafunzi hao walifariki dunia, ili viongozi wa juu wasifuatilie,” alisema Jongo.
Kwa mujibu wa Jongo ‘mchezo’ huo hufanywa kwa ushirikiano mkubwa kati ya walimu na wazazi ambao huwasafirisha wanafunzi walioolewa na kwenda kuwaficha katika vijiji vya mbali.
Naye Mariam Amrani mkazi wa Mgulani, akizungumzia tatizo la kuwazushia vifo mabinti kwamba aliwahi kusikia walimu wakifuta jina la mwanafunzi wa kike, kwa maelezo kwamba amefariki dunia.
Kauli ya walimu
Mwalimu Frank Manonge ambaye anafundisha Kemia katika Shule ya Sekondari Kizomla alisema kinachosikitisha zaidi ni namna baadhi ya wazazi wanawachukia walimu ambao wanapambana na vitendo vya kuwaoza wanafunziZaidi bofya hapa.
إرسال تعليق