Dimitar Barbatov |
WAKALA wa mshambuliaji wa zamani wa Manachester United, Dimitar
Berbatov, Emil Danchev amethibitisha kuwa nyota huyo atasalia kwenye
klabu yake ya sasa ya Fulham kwa msimu ujao.Mchezaji huyo mwenye
umri wa miaka 32 na aliyesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja ilidaiwa
alikuwa katika mipango ya kujiunga na klabu ya Zenit St Petersburg
waliovutiwa naye.Hata hivyo danchev alisema mkali huyo aliyewahi pia
kukipiga Tottenham kabla ya kutua United ataendelea kusalia katika
klabu hiyo."Ana mkataba wa mwaka mmoja zaidi na Fulham na atasalia hapa mpaka mtakata utakapoisha, " alisema wakala huyo na kuongeza;"Anajisikia
furaha hapa Fulham na anataka kubaki kwa mwaka mmoja zaidi. Hataki
kujadili suala la klabu nyingine kwa sasa. Hata kama kuna klabu
zinamhitaji binafsi anafurahia kuwepo kwake Fulham na anataka kusalia
hapa. Anataka kucheza angalau zaidi ya miaka miwili."Berbatov
ameifungia Fulham mabao 15 katika Ligi kuu kwa msimu wake wa kwanza
tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Manchester United.
Post a Comment