Bi Mery Mbilinyi ambaye ni diwani viti maalumu tarafa ya Lupalilo wilayani Makete ambaye kwa hivi sasa anasubiri adhabu yake kutoka CCM mkoa wa Njombe
Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wilaya Makete Jasel Mwamwala ambaye amepewa onyo kali
Katibu wa ccm wilaya ya Makete Miraji Mtaturu akitoa taarifa kwa waandishi wa habari
==========
Chama cha mapinduzi wilayani Makete kimewavua madaraka viongozi kadhaa wa chama hicho na wengine kupewa muda wa maangalizo wakiwemo makatibu na wenyeviti wa matawi na diwani wa viti maalumu Bi: Mary Mbilinyi ambaye bado anasubiri uamuzi kutoka katika ngazi ya mkoa ya chama chama cha mapinduzi
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Makete Bw Miraji Mtaturu Alisema kuwa adhabu hiyo kwa viongozi hao Imetolewa baada ya kujadiliwa katika kikao cha kamati ya maadili na usalama cha chama hicho na kupitshwa na kikao cha kamati ya siasa ya kilichofanyika hapo juzi na ndipo kuamua kutoa taarifa hiyo kwa umma kwini viongozi hao wamekuwa wakivunja sheria na taratibu za chama hicho cha siasa wilayani Makete
“Katika kikao cha kamati ya maadili na usalama ya viongozi wa chama cha mapinduzi kilichofanyika tarehe kumi na tatu mwezi juni kilijadili mienendo na tabia za baadhi ya wananchi na viongozi na kupitishwa na kikao cha kamati ya siasa waliobainika kuvunja sheria waliitwa na kujibu tuhuma zao na sisi tukajitosheleza na kuamua kuchukua uamuzi kama ofisi ya chama ngazi ya wilaya” alisema katibu huyo.
Akiendelea kuongea na Vyombo vya habari katibu Huyo Aliwataja viongozi ambao wamevuliwa madaraka kutokana na kukosa sifa ya kuwa viongozi baada ya Kukiuka maadili ya chama hicho kuwa ni katibu wa tawi la Luvulunge lililopo katika kata ya Isapulano Wilayani Makete Bw. Festo Chaula na katibu wa tawi la Mago lililopo katika Kata ya Lupalilo Bw.Creto Ngomano.
Aliwataja Viongozi waliopewa onyo na Kupewa Muda wa angalizo la miezi sita kuwa ni pamoja na mwenyekiti wa kijiji cha Luvulunge Bw. Daudi Mwamkinga na kiongozi mwingine ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa chama hicho Bw Jasel Mwamwala na kuongeza kuwa kiongozi huyo alikiri katika kikao cha kamati hiyo na ripota wetu alipopata taarifa hii alimtafuta kwa njia ya simu naye ailikana kuwa na taarifa ya kupewa onyo na chama hicho.
Pia Katibu huyo alimtaja diwani wa viti maalumu Katika chama cha mapinduzi wilayani Makete Bi. Mary Mbilinyi kuwa ni miongoni mwa viongozi ambao wamekuwa wakivunja maadili ya chama hicho cha mapinduzi ambaye bado anasubrli uamuzi utakaoendana na adhabu utakaotangazwa na chama hicho ngazi ya mkoa wa Njombe
Aidha aliwataka viongozi wa chama hicho kuwa makini katika utendaji wao wa kazi na kusema kuwa chama cha mapinduzi kina mtandao mrefu hivyo kina uwezo mkubwa wa kuwakamata viongozi ambao wanakiuka katiba ya chama hicho.
“Nawakubusha viongozi wa chama cha mapinduzi kwamba chama cha mapinduzi kina mkono mrefu kinafika hadi katika ngazi ya matawi na shina na kwamba mtu yeyote ataweza kuukwepa mkono wa chama hichi asiwezekurekebishwa ni jambo lisilowezekana “ alisema katibu huyo
Akizungumzia suala la mchakato wa katiba katibu huyo aliipongeza tume hiyo kwa ufanyaji wa kazi mzuri hadi uwasilishwaji wa rasimu hiyo ya katiba na kuwaunga mkono baadhi ya viongozi wa chama chake katika kipengere cha kuwepo kwa maraisi watatu na kusema kuwa kujiongezea gharama zisizo na msingi
“Naipongeza tume ya katiba chini ya Jaji mstaafu Warioba kwa kazi nzuri walioifanya hadi walipofilkia Lakini maoni ni ya kila mtu anaweza toa na kuhusu suala la kuwa na maraisi watatu hilo hata mimi nalipinga kwani ni kujiongezea gharama na jambo lingine ni suala la serikali ya shirikisho hakuna sababu ya kuwabebesha mzigo watanzania na vyama vya siasa….." alisema katibu huyo.
Na James Festo
Post a Comment