China yafikiria kuwekeza visiwani Zanzibar katika sekta ya viwanda vya mazao ya baharini.


617
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mkuu wa Divisheni ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Kimataifa  katika Idara ya Biashara ya Jimbo Heilongjiang Nchini China Bw. Li Leyu Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Idara ya Biashara kupitia kitengo chake cha ushirikiano wa Kiuchumi wa Kimataifa katika Jmbo la Heilongjiang Nchini China inakusudia kuwekeza katika sekta ya Viwanda vitakayozalisha  Mazao ya Baharini, hatua ambayo imekuja kufuatia mazingira mazuri yaliyopo ya Bahari ya Hindi iliyovizunguka Visiwa vya Zanzibar.
Mkuu wa Divisheni ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Kimataifa  katika Idara ya Biashara ya Jimbo hilo Bw. Li Leyu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Bw. Li Leyu aliyeuongoza Ujumbe wa Viongozi Wanne wa Idara hiyo amesema kwamba mradi huo wa uwekezaji utakwenda sambamba na utoaji taaluma kwa wavuvi wadogo wadogo ukilenga kuwa na  uzalishaji wa kimataifa  kwa kushirikisha pande zote mbili.
Mkuu huyo wa Divisheni ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Nje katika Idara ya Biashara ya Jimbo la Heilongjiag Nchini China, amefahamisha kwamba wataalamu wa kufanya utafiti wa kuendesha mradi huo watafika Nchini mara baada ya kuridhiwa pamoja na kukamilika kwa taratibu zilizowekwa za uwekezaji Nchini.

Post a Comment

Previous Post Next Post