Japan yaipiga jeki Tanzania katika sekta ya kilimo kwa mkopo wa shilingi bilioni 54.13 kwa ajili ya kuboresha kilimo cha umwagiliaji.

PST
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah(kushoto)  akifafanua umuhimu wa ujenzi wa miundombinu mipya ya kilimo cha umwagiliaji mpunga  hapa nchini jana jijini Dar es salaam  mara baada ya kusaini hati ya mkopo wa shilingi bilioni 54 kwa ajili ya kuendeleza zao la mpunga. Kulia ni  Balozi wa Japan nchini Masaki Okada. Wilaya 80 zinazolima mpunga zinatarajiwa kunufaika na mkopo huo kwa kujenga  miundo mbinu mipya na kukarabati ya zamani.(Picha na MAELEZO- Dar es salaam).
J2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah(kushoto)  na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia) wakisaini  hati ya makubaliano ya mkopo wa shilingi bilioni 54.13 jana jijini Dar es salaam  kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji mpunga hapa nchini. Wilaya 80 zinazolima mpunga zinatarajiwa kunufaika na mkopo huo kwa kujenga  miundo mbinu mipya na kukarabati ya zamani.
J1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah(kushoto)  na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo wa shilingi bilioni 54.13 jana jijini Dar es salaam  kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji mpunga hapa nchini. Wilaya 80 zinazolima mpunga zinatarajiwa kunufaika na mkopo huo kwa kujenga  miundo mbinu mipya na kukarabati ya zamani.
Japan imeipatia Tanzania mkopo wa shilingi bilioni 54.13 kwa ajili ya kuboresha kilimo cha umwagiliaji mpunga ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.
Makubaliano hayo yametiwa saini jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah  na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaki Okada ampapo Wilaya 80 zinazolima mpunga nchini zinatarajiwa kunufaika na mkopo huo.
Akizungumza mara ya kusaini makubaliano hayo Khijjah amesema kuwa fedha hizo zitasaidia kuboresha kilimo cha umwagiliaji wa mpunga katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kukarabati miundo mbinu ya zamani ya umwagiliaji na kujenga miundo mbinu mipya ikiwa na lengo la kuongeza uzalishaji wa zao hilo.
Amesema kuwa lengo la Serikali ni kupunguza uagizaji wa mchele kutoka nje ya Tanzania Japan ikiwemo, badala yake wananchi wajikite katika kuzalisha bila ya kutegemea mvua.
Ameongeza kuwa mpango huo ni sehemu ya Mkakati wa Serikali wa Kupunguza umaskini kwa wananchi na kukuza uchumi na hivyo kuboresha maisha ya wananchi kwa kuwahakikishia upatikanaji wa chakula cha kutosha.
Aidha Katibu Mkuu huyo amesema kuwa chini ya mkopo huo utasaidia kuongeza uzalishaji kutoka tani 3-4 kwa hekta hadi kufikia tani 6 katika mvuno mmoja.
Naye Balozi wa Japan nchini  Masaki Okada amesema kuwa karibu asilimia 75 ya Watanzania wamejiajiri katika sekta ya kilimo na hivyo fedha hizo ni muhimu kwa Tanzania katika kutekeleza malengo yake iliyojiwekea katika Kilimo kwanza.

Post a Comment

Previous Post Next Post