Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah(kushoto) akifafanua umuhimu
wa ujenzi wa miundombinu mipya ya kilimo cha umwagiliaji mpunga hapa
nchini jana jijini Dar es salaam mara baada ya kusaini hati ya mkopo wa
shilingi bilioni 54 kwa ajili ya kuendeleza zao la mpunga. Kulia ni
Balozi wa Japan nchini Masaki Okada. Wilaya 80 zinazolima mpunga
zinatarajiwa kunufaika na mkopo huo kwa kujenga miundo mbinu mipya na
kukarabati ya zamani.(Picha na MAELEZO- Dar es salaam).
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah(kushoto) na Balozi wa Japan
nchini Masaki Okada (kulia) wakisaini hati ya makubaliano ya mkopo wa
shilingi bilioni 54.13 jana jijini Dar es salaam kwa ajili ya
kuendeleza kilimo cha umwagiliaji mpunga hapa nchini. Wilaya 80
zinazolima mpunga zinatarajiwa kunufaika na mkopo huo kwa kujenga
miundo mbinu mipya na kukarabati ya zamani.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah(kushoto) na Balozi wa Japan
nchini Masaki Okada (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo
wa shilingi bilioni 54.13 jana jijini Dar es salaam kwa ajili ya
kuendeleza kilimo cha umwagiliaji mpunga hapa nchini. Wilaya 80
zinazolima mpunga zinatarajiwa kunufaika na mkopo huo kwa kujenga
miundo mbinu mipya na kukarabati ya zamani.
Japan
imeipatia Tanzania mkopo wa shilingi bilioni 54.13 kwa ajili ya
kuboresha kilimo cha umwagiliaji mpunga ili kuongeza uzalishaji wa zao
hilo.
Makubaliano
hayo yametiwa saini jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha Ramadhan Khijjah na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaki Okada
ampapo Wilaya 80 zinazolima mpunga nchini zinatarajiwa kunufaika na
mkopo huo.
Akizungumza
mara ya kusaini makubaliano hayo Khijjah amesema kuwa fedha hizo
zitasaidia kuboresha kilimo cha umwagiliaji wa mpunga katika maeneo
mbalimbali hapa nchini kwa kukarabati miundo mbinu ya zamani ya
umwagiliaji na kujenga miundo mbinu mipya ikiwa na lengo la kuongeza
uzalishaji wa zao hilo.
Amesema
kuwa lengo la Serikali ni kupunguza uagizaji wa mchele kutoka nje ya
Tanzania Japan ikiwemo, badala yake wananchi wajikite katika kuzalisha
bila ya kutegemea mvua.
Ameongeza
kuwa mpango huo ni sehemu ya Mkakati wa Serikali wa Kupunguza umaskini
kwa wananchi na kukuza uchumi na hivyo kuboresha maisha ya wananchi kwa
kuwahakikishia upatikanaji wa chakula cha kutosha.
Aidha
Katibu Mkuu huyo amesema kuwa chini ya mkopo huo utasaidia kuongeza
uzalishaji kutoka tani 3-4 kwa hekta hadi kufikia tani 6 katika mvuno
mmoja.
Naye
Balozi wa Japan nchini Masaki Okada amesema kuwa karibu asilimia 75 ya
Watanzania wamejiajiri katika sekta ya kilimo na hivyo fedha hizo ni
muhimu kwa Tanzania katika kutekeleza malengo yake iliyojiwekea katika
Kilimo kwanza.
إرسال تعليق