Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mkuu wa
Divisheni ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Kimataifa katika Idara ya
Biashara ya Jimbo Heilongjiang Nchini China Bw. Li Leyu Ofisini kwake
Vuga Mjini Zanzibar.
Idara
ya Biashara kupitia kitengo chake cha ushirikiano wa Kiuchumi wa
Kimataifa katika Jmbo la Heilongjiang Nchini China inakusudia kuwekeza
katika sekta ya Viwanda vitakayozalisha Mazao ya Baharini, hatua ambayo
imekuja kufuatia mazingira mazuri yaliyopo ya Bahari ya Hindi
iliyovizunguka Visiwa vya Zanzibar.
Mkuu
wa Divisheni ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Kimataifa katika Idara ya
Biashara ya Jimbo hilo Bw. Li Leyu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza
na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake
Vuga Mjini Zanzibar.
Bw.
Li Leyu aliyeuongoza Ujumbe wa Viongozi Wanne wa Idara hiyo amesema
kwamba mradi huo wa uwekezaji utakwenda sambamba na utoaji taaluma kwa
wavuvi wadogo wadogo ukilenga kuwa na uzalishaji wa kimataifa kwa
kushirikisha pande zote mbili.
Mkuu
huyo wa Divisheni ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Nje katika Idara ya
Biashara ya Jimbo la Heilongjiag Nchini China, amefahamisha kwamba
wataalamu wa kufanya utafiti wa kuendesha mradi huo watafika Nchini mara
baada ya kuridhiwa pamoja na kukamilika kwa taratibu zilizowekwa za
uwekezaji Nchini.
إرسال تعليق