Mabingwa
wa Ligi Kuu Tanzania bara 2012/2013 Young Africans ambao pia ni
Mabingwa watetezi wa kombe la Kagame. jumatatu wanatarajia kuanza
mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola Mabibo kujiandaa na
mashindano ya kombe la Kagame yanayotarajia kuanza Juni 18 mwaka huu
nchini Sudan.
Katika mashidano ya mwaka huu nchini
Sudan , Yanga imepangwa katika kundi C lenye timu za Express FC
(Uganda), Vitaloo FC (Burundi) na Ports FC (Djibout) ambapo kundi hili
litakua katika mji wa El Fashir Kaskazini mwa jimbo la Darfur.
Yanga
itaanza kutetea ubingwa wake Juni 20 dhidi ya timu ya Express ya
Uganda, kisha Juni 22 itacheza na Ports ya Djibout kabla ya kumalizia
mchezo wake wa mwisho katika makundi dhidi ya timu ya Vitaloo Juni 25
michezo yote ikifanyika katika uwanja wa El Fashir.
Mpaka
sasa klabu ya Yanga imefanikiwa kukamalisha usajili wa mchezaji Mrisho
Ngasa aliyekuwa akiitumikia Simba SC kwa mkopo akitokea timu ya Azam Fc
ambapo mara baada ya msimu kumalizika amejiunga Yanga kama mchezaji
huru.
Mara baada ya
mchezo wa mwisho wa kukamilisha ratiba Kocha Mkuu Ernie Brandts alitoa
mapumziko ya wiki mbili kwa wachezaji na benchi la ufundi kwa ajili ya
kupata nafasi ya kujumuika na familia zao, ndugu zao kabla ya kurejea
June 3 na kuanza maandilizi ya mashaindano hayo.
Young
Africans ambayo ilitwaa ubingwa wa VPL ikiwa na michezo miwili mikononi
inaanza mazoezi jumatatu asubuhi kuhakikisha inajiandaa vema kwenda
kushindana na kurudi na kombe hilo kwa kulitwaa kwa mara ya tatu (3)
mfululizo, ambapo mpaka sasa imeshalitwaa mara 5.
إرسال تعليق