MWANAMKE aliyetajwa kwa jina la Magreth Simon Nkwera ambaye andaiwa ni mtoto wa
kwanza wa Mnadhimu Mkuu wa kwanza wa JWTZ Brig Gen Simon Nkwera
amekamatwa kwa Mganga wa kienyeji akijaribu kutekeleza jaribio
la mauaji.
Kwa
mujibu wa taarifa ambazo zimepenyezwa kwa blogu hii pamoja na picha
zinasema kuwa mwanamke huyo alifumwa 'live' kwa sangoma akifanya mipango
ya kutekeleza mauaji kwa njia ya kishirikina dhidi ya watoto wa mumewe
na baadhi ya ndugu zake huko
Kibaha Maili Moja, Pwani.
Kwa
sasa mwanamama huyo anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Maili Moja
akisubiri kupandishwa kizimbani kwa kosa linalomkabili.
Mtuhumiwa akiwa ndani ya chumba cha mganga na mganga wake aitwae Yahaya tayari kwa mauwaji
Mtuhumiwa huyo akiwa ndani ya gari la polisi pamoja na mganga wake aitwae, Yahaya tayari.
Mtuhumiwa huyo akiwa ndani ya gari la polisi baada ya kukamatwa
Mtuhumiwa
akiwa anahojiwa na mzee wa ukoo wa shirima Ofisa Polisi Jeshi daraja la
Kwanza (woii mstaafu) Joseph Shirima mara baada ya kumkamata live kwa
sangoma.
Post a Comment