Aneth
Kushaba AK 47 akiongoza kikosi kazi cha Skylight Band kutoa burudani
katika usiku maalum wa Kiafrika kwa mashabiki wa Band hiyo Jumaa
lililopita ndani ya uwanja wao wa nyumba Thai Village- Masaki jijini
Dar. Usikose Ijumaa hii burudani kama kawaida
Mbunifu
wa Mavazi nchini Ally Rehmtullah alikuwa miongoni mwa mashabiki
waliohudhuria usiku huo maalum uliondaliwa na Skylight Band..Pichani
Ally Rehmtullah akiserebuka muziki wa Kiafrika na warembo aliombatana
nao.
Mashabiki
wa Skylight Band wakiburudika na muziki Kiafrika katika usiku maalum
uliondaliwa na Band hiyo Juma lililopita ndani ya kiota cha Thai
Village.
Rappa wa Skylight Band Sony Masamba akiwarusha mashabiki wake ndani kiota cha Thai Village Juma lililopita.
Raia wa kigeni wakionekana kuchizika na burudani ya Skylight Band.
Wadada wakijimwaga kwa raha zao.
Wewe burudani mwanzo mwisho…Usikose Ijumaa hii.
Mary Lukas akifanya yake jukwaani.
Palikuwa hapatoshi mpaka wengine walitamani kuvua mashati kwa utamu wa muziki.
Wapiga Solo na Bass wa Skylight Band wakiwajibika ni Allan Kisso na Chili Chala.
Aneth
Kushaba AK 47 alishuka jukwaani na kuwafwata wale walioketi na
kuwaimbia nyimbo nzuri za Kiafrika katika usiku maalum Juma lililopita.
Mashabiki wa Skylight Band wakishtua Style mpya ya kucheza Band hiyo inayofahamika kama “Yachuma Yachuma”.
Hapo sana wadada warembo wakishindina kunengua jukwaani huku mmoja wao akimpagawisha Joniko Flower.
Ukumbi ulifurika ni wewe tu ndio ulikosekana fanya Ijumaa hii uwepo ndani ya kiota cha Thai Village.
Picha na Moblog
Post a Comment