UNHCR inasema wakimbizi wameongezeka duniani |
Umoja wa mataifa unasema kuwa watu milioni 7.6, walifanywa kuwa wakimbizi mwaka 2012 huku idadi kamili ya wakimbizi wote duniani ikiwa juu zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka 1994
Takwimu mpya zilizotolewa na shirika la umoja wa mataifa kuhusu wakimbizi zimebaini kuwa idadi ya watu wanaolazimishwa kutoroka makaazi yao imepanda kwa kiasi kikubwa tangu mizozo ya Rwanda na iliokuwa Yugoslavia.
Inasema kuwa nusu ya wakimbizi millioni 45 ulimwenguni wanatoka kutoka mataifa ya Afghanistan,Iraq,Syria ,Sudan na Somalia.Shirika hilo linasema kuwa mwaka jana pekee watu millioni nane walikuwa wakimbizi huku mgogoro unaondelea Syria ukichangia pakubwa kupanda kwa idadi hiyo.
Shirika hilo la wakimbizi linasema kuwa kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi ni dhihirisho kuwa jamii ya kimataifa imeshindwa kusuluhisha mizozo iliopo na hata kuzuia mengine inayojitokeza
Ripoti iliyotolewa na kamishna mkuu wa shirika la kuwahudmia wakimbizi la UNHCR, Antonio Geteres anasema kuwa Syria ndio moja za sababu ya kuongezewka kwa wakimbizi duniani.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nchi zinazostawi zimewahifadhi 81% ya wakimbizi wote kote duniani ikiwa asilimia 11 zaidi ya idadi ilivyokuwa zaidi ya mwongo mmoja uliopita.
"takwimu hizi ni za kushtua sana. Zinaonyesha kiwango cha mateso wanayopitia watu pamoja na kuonyesha changamoto inazokabili jamii ya kimataifa kuzuia migogoro kwa wakati mzuri kwa wakimbizi hao,'' alisema Guteres wakati dunia ikiadhimisha siku ya wakimbizi duniani.
- bbc swahili
إرسال تعليق